MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kimataifa Malema 'avuliwa gamba' ANC
BOOKMARK THIS PAGE
Malema 'avuliwa gamba' ANC  Send to a friend
Friday, 11 November 2011 09:18


Mashirika ya habari, JOBURG, Afrika Kusini
KIONGOZI wa Umoja Vijana wa chama cha ANC kinachotawala nchini Afrika Kusini, Julius Malema (30) amesimamishwa wadhifa huo kwa miaka mitano .
Hatua hiyo imefikiwa jana, baada ya kamati  ya nidhamu ya chama hicho kutoa hukumu dhidi ya kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa kwa vijana wa chama hicho.

Malema ambaye siku za nyuma alikuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma lakini baadaye akamuasi, amekuwa katika malumbano makali na uongozi wa chama hicho na rais wake (Zuma).

Hata hivyo, katika kile kinachoonekana ni hatua mahususi ya kuzima uasi unaoweza kufanywa na Malema ndani ya ANC kutokana na nguvu na ushawishi aliyonayo kwa vijana, kiongozi huyo amesimamishwa na kuonywa kuwa iwapo ataonyesha kwenda kinyume na adhabu hiyo anaweza kufukuzwa katika chama hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya ANC, Derek Hanekom alisema tabia ya Malema imekishushia hadhi chama hicho na kwamba tabia yake siyo njia sahihi ya kuelezea hisia za kutoridhika na sera za chama.

Katika tuhuma hizo, Malema alishtakiwa pamoja na maofisa wengine watano, akishutumiwa kuchochea mgawanyiko na kuvunjia heshima ya chama hicho. 

Habari zaidi zilizopatikana jana zilidai kuwa,  huenda Malema akaondolewa  katika chama cha ANC.
Hata hivyo, inasemekana kuwa iwapo Malema atatimuliwa huenda ushawishi wake kuhusu atakayekuwa kiongozi wa nchi hiyo mwakani ukadidimizwa.
Malema ambaye hakuwepo kwenye makao makuu ya chama chake wakati hukumu hiyo ilipotolewa, amepewa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Kamati hiyo ya ANC imempata Malema na hatia ya kuvuruga mkutano wa ANC, kukivunjia hadhi chama hicho kwa kudai mageuzi ya utawala nchini Botswana na kuchochea migawanyiko ndani ya chama hicho.

Viongozi wengine wa Umoja wa Vijana wa ANC, akiwemo  msemaji wake Floyd Shivambu, wamesimamishwa katika nyadhifa zao kwa muda wa miaka mitatu.

Hata hivyo, kamati hiyo haikumpata Malema na hatia kwenye kosa la kuchochea ubaguzi wa rangi.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #3 2011-12-02 18:10
Maamuzi ya kamati kuu ya ANC nayaunga mkono kwani malema hana mamlaka ya kuingilia serikali ya Botswana kwa kuwa yeye si msemaji wake,huku kwetu kuna mtu anajiita NAPE naye hana muda mrefu atavuruga chama chake kwa kujifanya anajua sana.
Quote
 
 
0 #2 2011-11-29 11:26
SIYO SUALA LA NAPE, SEMA lOWASA, CHENGE, ROSTAMU AMESHAJIVUA.

NAPE NI MKJANA HODARI NAMI NAMPENDA, NI MPAMBANAJI WA KWELI ANAKIJUA CHAMA NA KUKIMPENDA CHAMA.
Quote
 
 
+3 #1 2011-11-11 12:53
Huku kwe2 kuna Nape.Vigogo hawapendi mabadiliko ndo maana wanawafanyia fitna na mizengwe kibao wanamapinduzi hao
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner