MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kimataifa Zuma: Tabianchi inatishia ustawi duniani
BOOKMARK THIS PAGE
Zuma: Tabianchi inatishia ustawi duniani  Send to a friend
Wednesday, 07 December 2011 20:55

MWANDISHI WETU, Durban
RAIS wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema mabadiliko ya hali ya hewa yameifanya dunia kuwa hatarini kwasababu yanasababisha madhara makubwa kwa binadamu.

Kutoka na hatua hiyo, Rais Zuma alitoa wito kwa nchi mbalimbali duniani kuhakikisha zinapambana ili kukabiliana na mabadiliko hayo makubwa.

Akizungumza jana mjini Durban, Afrika Kusini katika mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa, Rais Zuma aliziomba serikali za mataifa mbalimbali duniani kuheshimu juhudi zote za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Alisema tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa ni la dunia nzima, hivyo linahitaji ufumbuzi wa haraka zaidi katika hatua ya kukabiliana na tatizo hilo.

"Sisi wote tunakubaliana kuwa dunia ipo hatarini, na wote tumekubaliana kwamba lazima tufanye jambo kubwa ili kulitafutia ufumbuzi suala hili,” alisema Rais Zuma.

Katika mkutano huo ambao ulianza wiki Novemba 28 ambao unatarajiwa kumalizika kesho Ijumaa, umehudhuriwa na viongozi wa nchi 12 na mawaziri zaidi ya 100, unajadili masuala muhimu ambayo bado hayajapata maendeleo.
Awali, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wiki iliyopita, Rais Zuma alisema utatuzi wa suala la mabadiliko ya hali ya hewa unatakiwa kusaidia kupunguza umaskini barani Afrika.

Alisema, mabadiliko ya hali ya hewa yameathiri vibaya mazingira ya binadamu hususan nchi zinazoendelea duniani. Rais Zuma aliongeza, nchi nyingi za Afrika hazina uwezo wa kukabiliana na hali hiyo kutokana na kuwa nyuma kiuchumi.

Aidha, Mwenyekiti wa mkutano huo, Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, alielezea matumaini yake kwamba mawaziri wa nchi mbalimbali wataufanya mkutano huo uwe jukwaa la mazungumzo, ili kupata ufumbuzi wa njia za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, tatizo linalowaathiri binadamu wote.

Katika mkutani huo, nchi za Umoja wa Ulaya (EU) zinataka makubaliano mapya ambayo yataanza kutekelezwa mwaka 2020 yatafikiwa, ambapo Marekani na nchi zinazoendelea zenye maendeleo ya kasi ya kiuchumi zitakuwa na vigezo sawa vya kupunguza utoaji wa hewa za Carbon.

Lakini msimamo wa nchi zinazoendelea ni kuwa, kazi zinazotakiwa kupewa kipaumbele kwa sasa ni kuendelea kutekeleza malengo ya kipindi cha pili cha Makubaliano ya Kyoto, na nchi zilizoendelea kutoa msaada wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner