MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kimataifa ICC: Kenyatta, Ruto wana kesi ya kujibu
BOOKMARK THIS PAGE
ICC: Kenyatta, Ruto wana kesi ya kujibu  Send to a friend
Monday, 23 January 2012 20:09

NI KUHUSU MACHAFUKO YA UCHAGUZI MKUU 2007, NAFASI YAO YA KUWANIA URAIS SHAKANI, RAIS KIBAKI ANENA
Waandishi Wetu
MAHAKAMA ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), iliyoko The Hague, Uholanzi imewakuta na kesi ya kujibu watuhumiwa wanne kati ya sita walioshtakiwa kwa tuhuma za kuhusika katika machafuko yaliyoikumba Kenya wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2007.Waziri wa Fedha na Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, aliyekuwa Waziri wa Elimu ya Juu, William Ruto, Mkuu wa Utumishi wa Umma, Francis Muthaura na Mtangazaji wa Redio, Joshua Arap Sang watalazimika kujibu tuhuma zinazowakabili.

Akisoma uamuzi huo mbele ya jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji Ekaterina Trendafilova aliwataja watuhumiwa walioachiwa huru na mahakama hiyo kuwa ni aliyekuwa Waziri wa Viwanda, Henry Kosgey na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Jenerali Hussein Ali.

Uamuzi huo wa awali wa kesi ya watuhumiwa hao sita ambao ni maarufu kama Ocampo Six, ulitangazwa jana moja kwa moja kupitia vyombo vya habari, kutoka katika mahakama hiyo iliyopo mjini The Hague.

Hatua hiyo inaonekana kuwa pigo kubwa kisiasa kwa Kenyatta na Ruto. Waziri huyo wa Fedha, tayari alitangaza nia ya kuwania urais kupitia chama chake cha KANU mwaka huu na Ruto ameshatangaza dhamira ya kuwania ukuu huo wa nchi kwa chama ambacho atajiunga nacho baadaye.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007, Ruto alikuwa kambi moja ya chama cha ODM na Waziri Mkuu wa sasa, Raila Odinga na Mbunge wa Mombasa, Najib Balala, Mbunge wa Sabatia, Musalia Mudavadi na Waziri wa Ushirika na Maendeleo ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Gachoka, Joseph Nyaga. Lakini kundi hilo la watu watano lililofahamika kama The Pentagon lilisambaratika.

Katika vurugu hizo, watu 1,300 waliripotiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 500,000 wakapoteza makazi.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani hapo tangu mwaka jana na pande zote mbili; utetezi na mashtaka zilipata fursa ya kuwasilisha maelezo yao kabla ya uamuzi huo wa jana.Katika shtaka la kwanza, Ruto, Kosgey na Arap Sang, wanatuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, kuwatesa na kuwahamisha watu kwa nguvu.

Uhalifu huo unadaiwa kutekelezwa dhidi ya wafuasi wa chama cha Rais Mwai Kibaki cha Party of National Unity (PNU), katika maeneo kadhaa Mkoa wa Rift Valley.

Katika shtaka la pili, Kenyatta, Muthaura na Jenerali Ali nao walikuwa wanakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji, kuwahamisha watu kwa nguvu, ubakaji na mateso.Ghasia zilizuka baada ya Rais Kibaki kutangazwa mshindi kwenye uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali kati yake na Odinga.

Kutokana na ghasia hizo, jamii ya kimataifa iliwashinikiza Kibaki na Odinga kufanya mazungumzo kumaliza tofauti zao na kurejesha amani nchini humo.

Mchakato wa usuluhishi uliosimamiwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN), Kofi Annan na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ndiyo uliowezesha viongozi hao wawili kukubali kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa inayoongoza Kenya hadi sasa. Katika mchakato huo, Rais Jakaya Kikwete pia alitoa mchango mkubwa.

Kibaki: Mahakama za Kenya sasa zinaweza
Muda mfupi baada ya kumalizika kusomwa hukumu hiyo, Rais Kibaki alilihutubia Taifa na kumtaka Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo kuipitia hukumu hiyo ya awali kabla kesi ya msingi haijaanza kusikilizwa.

Ingawa hakusema moja kwa moja kwamba kesi hiyo irejeshwe Kenya, Rais Kibaki alisema baada ya vurugu hizo za Uchaguzi Mkuu, Kenya imepitia michakato mbalimbali ikiwamo marekebisho ya Katiba ambayo imebadilisha mfumo mzima wa uendeshaji mashtaka na jeshi la polisi.

“Mahakama zetu sasa zina uwezo wa kuziendesha kesi hizo na kutenda haki hasa baada ya marekebisho ya katiba yetu,” alisema Kibaki.

Ruto, Arap Sang kukata rufaa
Baada ya kutoka kizimbani, Ruto aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kusema kwamba ataka rufaa kupinga uamuzi huo.

Kauli kama hiyo ilitolewa pia na Arap Sang ambaye alisema uamuzi huo si sahihi akisisitiza kwamba hakuhusika wa machafuko hayo ya 2007.Habari hii imeandikwa na Hussein Issa na Daniel Mwingira kwa msaada wa vyombo vya habari vya kimataifa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Wednesday, 25 January 2012 00:09
 

Comments 

 
0 #12 2012-01-24 19:46
Quote
 
 
0 #11 2012-01-24 19:46
why this occurs only in africa continent.how about in europian.now take an opertunity even in western continent
Quote
 
 
0 #10 2012-01-24 17:30
not only those even those in high hierarchy are responsible.eg Mwai kibaki
Quote
 
 
0 #9 2012-01-24 17:25
Quoting Magessa Mulongo:
I feel sorry for the son of JOMO he wishes if he news of all this dirty games of politics,but anyway ICC is not custodian of standard is always subject to critisms,look at the us president Bush he was neccessarily as the matter of obligation to be there trialled,but because he is muzungu then they are not for the ICC,i really wonder if the Kenyans will allow those who are convicted to go ahead with the stupit court,let Kibaki play smart and throw away this ruling he will make history in Kenya as he did already
Poleni


Not again! The common song 'Blackman misery caused by white'.
W bush never kill his people neither caused tribal war in his USA.
These guys due to their presidential ambitions stirred violence which lead to blood shed in Kenya.
US might not be role model but are far better in protecting what they call theirs.
No Kibaki or any other African has power to oppose ICC- these guys shud stand on the dock!
Quote
 
 
-2 #8 2012-01-24 14:37
I feel sorry for the son of JOMO he wishes if he news of all this dirty games of politics,but anyway ICC is not custodian of standard is always subject to critisms,look at the us president Bush he was neccessarily as the matter of obligation to be there trialled,but because he is muzungu then they are not for the ICC,i really wonder if the Kenyans will allow those who are convicted to go ahead with the stupit court,let Kibaki play smart and throw away this ruling he will make history in Kenya as he did already
Poleni
Quote
 
 
+1 #7 2012-01-24 14:07
that good ocampo us tanzania we are suporse to learn from are fellow kenya
Quote
 
 
+1 #6 2012-01-24 12:28
Viongozi wa Serikali ya Tanzania wanaweza kujifunza kitu hapa.
Katika kila jambo ambalo wananchi wameonyesha kutoridhika na maamuzi na kuamua kuandamana jeshi la polisi limekuwa likitumiwa ku-supress mawazo ya wengi na mara nyingine watu wamekuwa wakipoteza maisha.

Serikali yaweza kuudhulumu umma wanaouongoza kwa kutumia 'Nguvu ya Dola' lakini iko siku mtawajibishwa.
Quote
 
 
+1 #5 2012-01-24 11:35
Akiagizwa na marekani atakuja

Quoting Julius Kimathi:
Tunakuomba Ocampo, uje Tanzania 2001 kulifanyika mauaji pia Zanzibar, Unguja na Pemba watu wasio na hatia waliuliwa kutokana na maandano ya amani kabisa, Watuhumiwa wapo ni Mkapa, Kizuguto, Mwinyi na Mahita, pamoja na Viongozi wa Vikosi vya SMZ, JKU, KMKM na VALANTIA. Bwana Ocampo watu zaidi ya 3000 walikufa Unguja na Pemba kupitia mauaji hayo mashahidi wa kutosha wapo, tafadhali uje na huku.
Quote
 
 
0 #4 2012-01-24 11:27
Wewe unayejiita Kimathi, huyo Mzee Mwinyi alifanya nini kwenye hayo mauaji? Hakuwa Rais wala na post yo yote ya maamuzi kwa nini umemuonea?

Wacha kutaja majina ya watu kwa utashi wako tu. Mbona Karume aliyekuwa mkuu wa nchi umemuacha?
Quote
 
 
0 #3 2012-01-24 09:20
serekali ya kenya ilifanya makosa kuku bali kesi hiiifunguliwe katika mahkama ya icc wengeiga mfano wa afrika kusuni kwakuridhiana yakaisha sasa nahisi wataitumbwikiza tena katika sias za chuki nauhasama na kuendeleza wimbi la mauwaji
Quote
 
 
0 #2 2012-01-24 07:59
Tunakuomba Ocampo, uje Tanzania 2001 kulifanyika mauaji pia Zanzibar, Unguja na Pemba watu wasio na hatia waliuliwa kutokana na maandano ya amani kabisa, Watuhumiwa wapo ni Mkapa, Kizuguto, Mwinyi na Mahita, pamoja na Viongozi wa Vikosi vya SMZ, JKU, KMKM na VALANTIA. Bwana Ocampo watu zaidi ya 3000 walikufa Unguja na Pemba kupitia mauaji hayo mashahidi wa kutosha wapo, tafadhali uje na huku.
Quote
 
 
0 #1 2012-01-24 04:52
Kama mtu hakuhusika katika machafuko hayo hakuna haja ya kuweweseka subiri kesi ianze upande wa mashitaka utaleta mashahidi wake na upande wa utetezi utapata fursa ya kujitetea kwa kujibu mashitaka na kupeleka mashahidi baada ya hapo kazi ya majaji waliobobea kwenye sheria kuchambua pumba na mchele.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner