MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kimataifa Ki Moon: Dk Migiro ameomba kupumzika
BOOKMARK THIS PAGE
Ki Moon: Dk Migiro ameomba kupumzika  Send to a friend
Thursday, 26 January 2012 21:06

NEWYORK, Marekani
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo,  Asha Rose Migiro ameomba mwenyewe kustaafu.Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijiji New York, Marekani, Ki Moon alisema hata hivyo Dk Migiro ataendelea kuwapo kwenye ofisi za umoja huo, akiratibu shughuli mbalimbali hadi Juni mwaka huu.

 Alisema mbali na Dk Migiro, mwingine aliyeomba kuacha kuutumikia umoja huo ni Vijar Nambiar ambaye ni Mkuu wa  Ofisi yake.

 “ Kama mlivyotangaziwa mwishoni mwa mwaka jana kuhusu mabadiliko  yanayotarajiwa kufanyika katika nafasi za  watendaji waandamizi. Ningependa kuongezea na kuwajulisha kwamba, Naibu Katibu Mkuu,  Dk Migiro  na Vijar Nambiar wamewasilisha   kwangu maombi  yao ya kutaka kuachia nafasi zao  ili kuniruhusu  kuunda timu mpya ya  maofisa waandamizi nitakaofanya nao kazi katika  awamu  ya pili ya  uongozi wangu,” alisema Ki Moon.

 “Ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati  kabisa kwa  Naibu Katibu Mkuu, Dk Asha- Rozi Migiro,  kwa uamuzi wake huo, na kwa kazi nzuri na ushirikiano mkubwa na usio na shaka wala doa  alionipatia katika kipindi chote cha miaka mitano iliyopita akiwa msaidizi wangu wa karibu,” alisisitiza.  

Alisema Dk Migiro alimpa  ushirikiano mzuri mno na kumshauri kwa busara huku akijituma kwa uadilifu mkubwa katika kukabiliana na changamoto nyingi  zinazoukabili Umoja wa Mataifa.


Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, aliyasema hayo baada ya  kuainisha mpango kazi na vipaumbele vyake katika miaka mitano ya muhula wa mwisho ya uongozi wake Kwa mujibu wa Ki Moon watendaji wengine watakaondoka ni wa Idara za Utawala, Maendeleo, Huduma za Mikutano,  Habari,  Ofisi ya Upokonyaji wa silaha,  na Mshauri wa Masuala ya Afrika.

 Wengine ni   wasimamizi  wa  Idara za Uchumi za Afrika na Ulaya,   waratibu wa  mifuko ya maendeleo na Idadi ya watu  UNDP na UNFPA. 


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #19 2012-02-13 22:09
acha mama arud nyumbani apumzike kwan ametumikia dunia kwa kipindi kirefu. arudi ajiandae na uchaguzi mkuu 2015.
Quote
 
 
+4 #18 2012-02-02 08:59
umedanganywa mama sana, hizo ndoto za uraisi sio halali kwako.labda ujivue gamba mapema na tujue msimamo wako
Quote
 
 
0 #17 2012-01-29 18:05
hongera mama, welcome back home
Quote
 
 
0 #16 2012-01-29 18:01
hebu tupeni uhalisia wa kuachia ngazi kwake, au ndio kama alivyofanya mangura ccm? ok karibu mama njoo ujiandae uchukue urais wa TZ 2015 zamu yenu akina mama, I hope unaweza mama
Quote
 
 
+1 #15 2012-01-29 10:55
kwa kweli kila kitu kina mwanzo na mwisho wake hebu tukae tufikirie kama waumini kuwa Mungu akitaka uwe utakuwa tu hata kama kwa nusu dakika kwa maana kwamba tusitengeneze maneno ambayo hayana ukweli kumuweka wanadamu mwenzetu midomoni kwani mtu kustaafu ni kosa !!! kubwa tumuombee mapumziko mema nata kama akirudi nyumbani akipangiwa kazi nyengine basi tumpe mashirikiano hakuna mkamilifu kwa kila kitu ila Mungu ndie mwenye uwezo wa kujua. Watanzania ni wastarabu na wakarimu tuache hizi tabia za kuiga kwa kila jambo kuanza kudhani tu.Kila mtu ana haki katika hii dunia ya kuishi na kufanya anachokipenda
Quote
 
 
+2 #14 2012-01-27 14:41
Jiunge Chama cha demokrasia Makini kama unataka Urais
Quote
 
 
+4 #13 2012-01-27 13:38
kuna nini nyuma ya pazia? ban kuwa mkweli kwa sababu hujaonyesha kusikitishwa na kuondoka kwa asha bali kinafiki unampongeza, 2siwaamini sana hawa wa2 weupe mara nyingi they don mean what they say wanapenda sana kujiangalia wao kwanza,
Quote
 
 
0 #12 2012-01-27 12:47
amejitahidi kufanya kwa kadiri alivyojaliwa na mwenyezi mungu,hongera mama kwa [NENO BAYA]liza kazi hyo bila kashfa,karbu nyumbani
Quote
 
 
+4 #11 2012-01-27 11:59
Anataka Urais ndio maana ameomba kuacha kazi UN!
Quote
 
 
+4 #10 2012-01-27 11:59
Mama karibu tena nyumbani. Tunashukuru umetuwakilisha na kuweka historia ya Tanzania kwenye ulimwengu.
Quote
 
 
0 #9 2012-01-27 10:39
RUDI MAMA RAIS MTATAJIWA
BILA WEWE CMM HAISHINDI NGÓ
Quote
 
 
0 #8 2012-01-27 09:30
Dada yangu hapo umechemsha kama wamekudanganya utakuja kugombea urais na kushinda hizo ni ndoto za Abunuasi,hapa swala sio mtu,swala hapa ni hicho chama ulichopo cha magamba ndo tumekichoka na sera zake za kuongeza umasikini nchini kwa wachacahe kujilimbikizia mali na kufaidi rasilimali za nchi kwa kukingiwa kifua,hatutaki tena huo mchezo
Quote
 
 
+4 #7 2012-01-27 09:16
Hongera Dk. Migiro kwa kazi nzuri uliyoifana na kwa heshima uliyotupatia watanzania katika jamii ya kimataifa...Mungu wa mbinguni akupe nguvu na maisha marefu...karibu nyubani tz tujenge nchi yetu na kupiga vita ufisadi
Quote
 
 
+4 #6 2012-01-27 09:04
Hongera sana Dr Migiro kwa kufanikiwa kupata wadhifa huo japo kwa miaka mitano. ila nilkupe pole vilevile kama utakuwa umeamua kupumzika ukiwa na lengo la kuja kugombea urais Tanzania 2015. kama kuna wanaokushauri hivyo basi wanakudanganya kwani nchi hii kwa sasa imebaki ni ya mafisadiwenye uchu wa madaraka wasiokubali kushindwa na sasa wanapita makanisani kuusaka uraisihivyo kuufanya uwezekano wa wewe kupewa nafasi kuwa mdogo na hata ukipewa nafasi hiyo bado watakuchakachua kwenye uchaguzi mkuu ikiwa ni katika kulipiza kisasi na bahati mbaya zaidi wewe ni mmoja wa wanachama kinachoonekana wazi kupoteza mwelekeo. kama kweli nia yako ni kutaka urais Tanzania jiandae kukabiliana na hali ngumu zaidi ikiwa ni pamoja na vitisho pia matumizi makubwa ya pesa. karibu tanzania. karibu nyumbani
Quote
 
 
+2 #5 2012-01-27 08:20
Karibu nyumbani Dr. Rose, Rais Mtarajiwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2015. Uadilifu wako unahitajika sana kuisafisha nchi hii, kuondoa makundi yasiyojenga nchi na kwa busara zako watanzania waona mbali tunaimani hutawasahau wachapakazi kama Mh. Edward Lowasa, Mh. John Makufuli, Boys and Girls of the Nation/Nguvu ya Umma katika kuhakikisha tunu za taifa zinawanufaisha watanzania wote. Karibu mama!!!
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner