MwanzoContactsEmail
Home Habari Matukio ya kusisimua Rombo kama Loliondo
BOOKMARK THIS PAGE
Rombo kama Loliondo  Send to a friend
Thursday, 17 March 2011 20:25

Daniel Mjema, Moshi
 

Ni siku za mwisho? Hili ndilo swali lililoanza kuumiza vichwa vya watu baada ya kijana mmoja kuibuka wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro na kudai ameoteshwa dawa ya ajabu na Bikira Maria inayotibu magonjwa sugu ukiwamo Ukimwi.Kama ilivyo kwa mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambikile Mwasapile wa Loliondo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, kijana huyo naye amekuwa akitoa tiba kwa sh500.
 
Kwa imani ya waumini wa Kanisa Katoliki Duniani, Bikira Maria ni mama wa Yesu ambaye anaaminiwa na waumini wa Kanisa hilo na hata katika sala jina lake ndilo linalotumika zaidi huku  wakiamini kuwa Yesu ni mtoto wa Mungu.Habari za uhakika kutoka eneo la Customs katika mji mdogo wa Tarakea, mpakani mwa Kenya na Tanzania, zilimtaja kijana huyo ambaye sasa anajiita Nabii, kuwa ni Hilary James Kitwai (28), kutoka wilayani Babati.
 
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Tarakea, Kitwai alisisitiza kuwa dawa hiyo ameoteshwa na Bikira Maria na Yesu na kwamba inatibu Ukimwi, Saratani, Kisukari, Shinikizo la Damu, Figo, Pumu na maradhi ya maumivu.

"Walinitokea kwenye ndoto wakanionyesha huo mti na waliniambia kwa sasa tuko wawili tu Tanzania, lakini huyo mwenzangu simfahamu. Mimi natoza Sh500 lakini katika hiyo pesa yangu na familia yangu ni Sh300 tu,"alidai.
 
Kitwai ambaye amekuwa gumzo katika mji wa Tarakea, alisema anakabiliwa na changamoto kubwa katika kuwahudumia wenye mahitaji kwa kuwa hana msaada na kuomba serikali imsaidie kumpatia wahudumu.
 
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari  kutoka wilayani Rombo, tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimemzuia kwa muda, kijana huyo kutoa tiba inayofanana na ya mchungaji Mwasapile na kuitisha sampuli za mizizi anayoitumia.
 
Kijana huyo ambaye ni fundi baiskeli kwa miaka mingi katika eneo hilo, aliibuka Jumatatu wiki hii na kuanza kutoa tiba kwa kutumia kikombe na tayari watu takribani 100 kutoka Kenya na Tanzania wamekunywa dawa yake.
 
"Anadai kuwa ameoteshwa na Bikira Maria na alielekezwa huo mti ambao una utomvu na kuanzia juzi (Jumatatu),watu kama 100 hivi walishakunywa dawa hiyo ambayo wenyeji wanadai mti wake ni sumu,"kilidai chanzo chetu.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Tarakea, Motamburu,  Kimario, alilithibitishia Mwananchi kuwapo kwa kijana huyo.

Kimario alisema yeye binafsi, Ofisa Afya na Ofisa Usalama wa Taifa, walifika nyumbani kwa kijana huyo juzi na kumfanyia mahojiano."Tulimhoji akasema alitokewa na Bikira Maria na Yesu ambao walimwonyesha mti huo ambao upo katika Mto Tarakea na walimwambia yupo mmoja tayari anayetibu maradhi sugu na kwamba yeye atakuwa wa pili,"alisema mtendaji.
 
Kwa mujibu wa mtendaji huyo, kijana huyo aliwaeleza kuwa baada ya Babu wa Loliondo na Yeye, bado atatokea mtu wa tatu ambaye naye ataoteshwa dawa za kutibu maradhi hayo na baada ya hapo Yesu mwenyewe atakuja duniani.
 
"Tulimuuliza kama ameshatoa dawa hiyo kwa watu mbalimbali akasema alianza kutoa Jumapili na watu kama 20 hivi walikunywa na alitupa vipande vya miti viwili vya dawa hiyo na tumevikabidhi kwa uongozi wa juu,"alisema Kimario.
 
Kwa mujibu wa Kimario aliyekuwa akimkariri kijana huyo, alisema 'nabii' huyo ameamua kutoendelea kutoa tiba hiyo hadi hapo serikali itakaporidhia na kwamba kwa sasa anamuomba Mungu ampe maono zaidi juu ya dawa hiyo.
 
Wananchi walioongea na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo, wameitahadharisha serikali kuwa makini na watu wanaojiita ni manabii vinginevyo wananchi wanaweza kukumbwa na maafa ya kunywa sumu bila kujua.
 
Wananchi hao wameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwajibika kikamilifu kwa kuzuia matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa kutokuwa na madhara.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Anthony Tesha ambaye pamoja na kukiri kusikia habari hizo lakini alisema anaviachia vyombo husika kufuatilia jambo hilo.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #45 2011-03-25 16:10
duh
Quote
 
 
0 #44 2011-03-21 16:44
Msihofu wandugu. Hiyo ni mitishamba. Na isitoshe bado unahitajika angalao kuamini kuwa dawa uliyokunywa inaponya ili kuiona nafuu(placebo effect). Bado suala la imani liko pale pale. babu anawashinda wahubiri wanamaombi kwani tiba yake yeye inashikika na kuonekana kwa macho. Nasema hivo kuwakumbusha kuwa binadamu sote sisi si tofauti sana na Tomaso wa enzi zile za yesu. Hivo kunyweni dawa, wala msihofu, inachimbwa kutoka kwenye mti uliopo siku zote na wala haijafwatwa kuzimu!!! mnachohofu nini sasa?
Quote
 
 
0 #43 2011-03-20 21:48
achani utape sasa vimezidi huyo wa rombo ni msanii
Quote
 
 
0 #42 2011-03-19 10:22
Quoting Desideri Chuwa:
"na hata katika sala jina lake ndilo linalotumika zaidi"
Daniel Mjema...Je una hakika na maneno haya uliyoandika. naomba editorial board ya Mwananchi iwe serious kidogo katika kuandika habari!


Kweli hili lilinipa shida sana, kwani kuna ukweli gani kuwa Wakatoliki sala zao zote lazima kuwe na jina la Maria? Huyu Mjema asiandike tu hata asivyo vifahamu kwani hayo si maneno ya huyo kijana bali ni ya mjema kunogesha lakini huku ni kupotosha. Sisi tunamheshimu sana mama Maria na ni mama wa Mungu na ni muombezi wetu.
Quote
 
 
0 #41 2011-03-19 08:30
jamani huyu kijana kasoma na rafiki yangu darasa moja familia yao ni ya kitapeli tangu enzi na enzi, hivyo ni tapeli mkuu jamani asijemsingizia Mungu.tujihadhari watanzania. hiyo ni mbinu tu serikali itambue, atafute mbinu nyingine hyo ni tapeli
Quote
 
 
0 #40 2011-03-19 00:10
Jamani na mimi niliwahi kuoteshwa nikiwa mdogo...bei yangu 275/- tu. ukitoa 500 chenji inarudi
Quote
 
 
0 #39 2011-03-18 20:49
Kumbe huu ni ujasiriamali! Tujiandae kusikia wengi kila kona ya nchi. 500/- tu si haba na hali ya maisha ilivyopanda, uongo mwanawane, angalau wakitokea 10 kila siku hukosi cha mkono kuingia kinywani!
Quote
 
 
0 #38 2011-03-18 20:41
Huyu kijana mbona haeleweki? Mara "Walinitokea kwenye ndoto wakanionyesha huo mti na waliniambia kwa sasa tuko wawili tu Tanzania, lakini huyo mwenzangu simfahamu." Mara "Kwa mujibu wa mtendaji huyo, kijana huyo aliwaeleza kuwa baada ya Babu wa Loliondo na Yeye, bado atatokea mtu wa tatu ambaye naye ataoteshwa dawa za kutibu maradhi hayo na baada ya hapo Yesu mwenyewe atakuja duniani.
" kweli [NENO BAYA] ndio waliwao.........
Quote
 
 
0 #37 2011-03-18 19:55
ELIMU NI MUHIMU SANA. SASA INAONYESHA KUWA NCHI YEYOTE YENYE ELIMU WATU WAKE HAWANA U[NENO BAYA] WA NAMNA HII .PENYE ELIMU DUNI NDIO [NENO BAYA] WANATOKEZA NA KUWAOKOTA WENZAO WENYE KUWAPIGIA DEBE.NAKUMBUKA WAKATI FULANI ALIWAHI KUTOKEA MTOTO WA MIUJIZA TANZANIA WAKIMWITA SHEHE SHARIFU.ALIPELEKWA NCHI ZA NJE KAMA MTOTO WA MIUJIZA ALIPOWEKWA KITI MOTO.MAJIBU TULIOPATA KUWA NI MTOTO WA KAWAIDA HAKUNA MIUJIZA YOYOTE.
Quote
 
 
0 #36 2011-03-18 19:30
Kweli Tanzania Tunaishi kwenye giza na shida. Sasa miradi na dili zimepelekwa kwenye nguvu za giza.Biashara .maradhi.na sasa watu wanadai Unabii .kweli ipo serikali au ndio uhuru wa kila mtu kufanya anachotaka hata kama anataka kuanzisha DINI mpya ni ruhusa kutoka SERIKALI YA jamhuri Tanzania.
Quote
 
 
0 #35 2011-03-18 19:15
Habari za chini kwa chini zinasema kuwa, baadhi ya wachungaji wamekuwa na wasiwasi kuhusu huduma ya Babu Mwasapile wakiamini kuwa, kama ushuhuda wa watu kupona utakuwa mkubwa, wao hawana chao kwa vile wameshawaombea sana watu lakini matatizo yao yako pale pale.
Wakati huo huo, kuna ushahidi wa kutosha kuwa, baadhi ya waumini walio kwenye foleni ya kufika kwa babu kupata kikombe wamekuwa wakitoa ushuhuda namna walivyoombewa katika makanisa ya kilokole lakini bila mafanikio na ndiyo hao hao sasa wanalalamika juu ya babu huyu.
“Hofu ya wachungaji hao ipo kwenye vituo vyao vya maombezi vilivyofurika mjini, wakati huu vitabaki tupu, watu wanakwenda Loliondo na hawatasubiri tena maombezi.”

Kauli za wachungaji hao ni ishara kwamba, hakuna mwananchi anakayeweza kusubiri muujiza wa kupona ugonjwa kwa kutumia maneno ya jukwaani wakati kuna babu Loliondo anatibu bila mahubiri ya muda mrefu.
Quote
 
 
0 #34 2011-03-18 18:07
jamani sasa huyu kijana anatisha kweli! sasa inamaana kuja kwa yesu si ndiyo mwisho wa dunia? tafadhali wewe kijana nenda kaote tena, bila shaka uliota sivyo,eti atatokea mganga wa tatu na hapo yesu atakuja!!!!!! please hatutajianda kwa yesu kuja hivi karibuni! tafadhali nenda kalale tena labda utaota vinginevyo!!! NABII WA ROMBO!!!
Quote
 
 
0 #33 2011-03-18 16:37
Huu utakuwa uhuni sasa,watu wengi washakuwa desparate na haya magonjwa sugu iko siku tutanyweshwa sumu na nina uhakika"manabii" hawa wataongezeka na wengine watadai wanatibu kwa mia mbili tu!!!
Quote
 
 
0 #32 2011-03-18 15:17
Sasa watu mnamshambulia nabii wa babati na kumtetea nabii wa Loliondo, ni nani aliyewathibitis hia kwamba huyo alipota mafunuo ya kweli? Kama naye anatoa mti wenye sumu kali na watu hawafi hamuoni kuwa mafunuo yao yana asili moja? Angalieni, kwani shetani naye anauwezo wa kujigeuza kuwa malaika wa nuru. Mtawatambua kwa matunda yao, Mat 10:16. Wote wanaokunywa kikombe wanapaswa kumgeukia Mungu wa kweli, vinginevyo....... Imani tu haitoshi. Kwanza imani ipi? Kwamba kikombe kinaponya? Au Yesu anaponya? Haitoshi tu kuambiwa uwe na imani.
Quote
 
 
-1 #31 2011-03-18 14:43
,,Jamani,watu inabidi wawe makini na haya mambo,Mchangaji wa Loliondo amekatazwa kutoka kule na amepewa sharti la kutoa dfawa kule alipo,iweje tena Mung huyo huyo amwagize mwingine Rombo?na kwa gharama ile ile? ninachojua Bikira Mariam sio nabii wala mtume,angesema ni Yesu amemtokea labda ningefikiria ila kwanini iwe na pesa,Yesu anasema nimewapa bure nanyi toeni bure,pia jina la YESU pekee ndio lenye uweza wa kufanya makuu na sio miti shamba,kinachot okea sasa nikuwafanya watu wa amini ktk vitu badala ya kumwamini MUNGU!..Miujiza mingapi makanisani inafanyika ikiwemo kuponywa ukimwi,cancer na mingineyo mbona haitangazwi hivyoo?,,mimi nina mashaka na haya yanayotokea,she tani amegundua waafrica wanamini vitu mfano hirizi,chale n avinginevyo naye anaamua kutumia vitu hivyo hivyo kupotosha na kuwafanya watu waache kumwamini MUNGU nakufata vitu vidanganyavyo!, ,
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner