MwanzoContactsEmail
Home Habari Matukio ya kusisimua Bibi harusi ashikwa uchungu, ajifungua kanisani Muheza
BOOKMARK THIS PAGE
Bibi harusi ashikwa uchungu, ajifungua kanisani Muheza  Send to a friend
Thursday, 11 August 2011 21:16

Mwandishi Wetu, Muheza
BIBI harusi aliyefahamika kwa jina la Mariam Shabani, ameshikwa na uchungu wa kujifungua kanisani wakati akifungishwa ndoa na mchumba wake, aliyefahamika kwa jina la Deo Massawe.Tukio hilo lilitokea juzi Kanisa Katoliki lililopo maeneo ya Majengo Shimoni, wilayani Muheza, huku umati wa watu ukiwa umejaa ndani ya kanisa hilo ukiisubiri kufungwa kwa ndoa hiyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa hilo, wakati Padri Martin Kihiyo, akiendelea na misa ya kufungisha ndoa hiyo, ghafla bibi harusi akiwa amevaa vazi rasmi la harusi, alianza kupiga kelele akidai anasikia uchungu wa kujifungua.

Hata hivyo, baada ya bibi harusi huyo kupiga kelele, Padri Kihiyo alisitisha misa hiyo  na Mariamu kuchukuliwa haraka na kuwekwa kwenye gari huku akiwa hajiwezi hadi Hospitali Teule Muheza.Pia, Mariamu anafahamika kwa jina la Sada Shabani, baada ya kufikishwa hospitali alipelekwa chumba cha kujifungulia huku akiwa na vazi lake la harusi.

Baada ya kuhudumiwa Mariamu, alijifungua mtoto wa kike na kulazwa wodi ya Azimio wanakolazwa wazazi.
Mmoja wa muuguzi hospitalini hapo aliyeomba asitajwe, alisema bibi harusi huyo alijifungua njiti akiwa na miezi saba.Kwa upande mwingine, kwenye ukumbi ambao ulikuwa umeandaliwa kwa sherehe ya  harusi hiyo, watu walikuwa wamekaa ndani wakisubiri maharusi bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea.

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo bwana harusi alilazimika kufunga ndoa na msichana mwingine wa pembeni kwa niaba ya bibi harusi, ili kuhalalisha sherehe hiyo huku bibi harusi mwenyewe akiwa hospitali analea.

Inasemekana Mariamu alianza kusikia uchungu akiwa saluni na aliwaeleza baadhi ya watu, lakini walimjibu kuwa huo ni woga wa harusi.Katika hatua nyingine, mbuzi wa ndafu aliyekuwa ameandaliwa alianguka chini kwenye mchanga.

Baadhi ya Wakristo walisikitishwa na tabia ya viongozi wa dini kuendelea kuwafungisha ndoa watu ambao wake zao wana mimba kwamba, ni aibu.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #24 2011-08-23 08:49
JAMANI POLE SANA BIBI HARUSI USIWAZE SANA MIMI MWENZIO ILINITOKEA USIKU WA KUAMKIA SEND OFF NIKAJIFUNGUA HIVYO HIVYO NJITI NA ASUBUHI YAKE KUKAKUCHA JIONI YAKE NIKAENDA KWENYE UKUMBI WA SEND OFF KWA HIYO USIUMIE SANA LA MUHIMU LEA KINJITI CHAKO BAADA YA HAPO KAFUNGE NDOA HUYO ALIYESIMAMA BADALA YAKO USIKUBALI KABISA ASIJE AKAKUIBIA MUME WANAOKUPONDA WAACHE WAENDELEE KUSEMA HAKUNA AMBAE SASA HIVI ANAOLEAWA BILA KUCHAKACHULIWA SEMA NI KWA SABABU HAWABEBI MIMBANA WENGINE WANATOA ILI WAFUNGE HARUSI
Quote
 
 
0 #23 2011-08-12 20:32
saada shabani bado mengi utayapata leo kanisani kesho motoni kwa laana yakutumia jina kuwa kafiri laana tulallah
Quote
 
 
0 #22 2011-08-12 19:22
Sasa aliyetoa kiapo ndiye mke halali na sio vinginevyo. Huwezi kula kiapo kwa niaba ya mtu ambaye hayupo na hajakuidhinisha ufanye kwa niaba yake. Au huyo mshichana wa pembeni ilikuwa nyumba ndogo ya bwana harusi tangu siku nyingi? Alilazimishwa kumuoa huyo Mariamu wakati anampenda huyo wa pembeni?
Quote
 
 
0 #21 2011-08-12 18:50
Katika Kanisa Katoliki hakuna cha kufunga ndoa kwa niaba. Huyo bwana harusi kama kafunga ndoa na binti aliyekuwa pembeni maanake ndiye MKE wake na wala siyo yule aliyejifungua. Uislam ni kawaida kufunga ndoa kwa niaba lakini siyo ukristu kwa madhehu asilia ya Katoliki, Lutheri, Anglikana, Moravian, Menonnite. Kwa wale wanakinyakulia uchungaji na uaskofu kama Kakobe na kunyima waumini kwenda hospitali inawezekana. Tunaomba Askofu wa Jimbo la Tanga (Katoliki) atufafanulie juu ya hili tukio.
Quote
 
 
0 #20 2011-08-12 18:24
Nimetilia shaka hii habari ya binti kufunga ndoa kwa niaba ya bi harusi. Linahitaji ufafanuzi.
Quote
 
 
+1 #19 2011-08-12 14:47
za mwizi ni arubaini hiyo ni ndoa au nini si bora mngeacha sasa ona mambo yenu yalivyowekwa hadharani aibu tupu.
Quote
 
 
+1 #18 2011-08-12 13:43
Hiyo ni noma na kali ya mwaka,cjui 2seme dini imekufa ama shetani kakamata dunia.Ni vp mchakachuane then ndoa ifuate.Tena padri bila woga .....
Quote
 
 
0 #17 2011-08-12 13:08
iwekwe wazi...kwamba kuna harusi za wajawazito
wasio wajawazito
wenye watoto tayari
ili sasa iwe wazi kwamba kuna harusi za aina hiyo ili aibu flani flani zisiendelee kutokea na akuppotosha maadili ya jamii.

wachungaji aua mapadre,maimamu wawe makini ili kuzuia aibu kama hizi
Quote
 
 
0 #16 2011-08-12 12:25
Imefika wakati kwa viongozi wa dini kuwa wakali kwa waumini wao mara wanapobainika kwamba maharusi watarajiwa tayari walikwisha kuwa na mahusiano ya kindoa ambayo yamepelekea ujauzito.Ni vema wakawashauri kusubiri mpaka mtoto atakapozaliwa na baadae waje kufunga badala ya kufumbia macho matukio hayo,ambayo yataleta aibu kwa kanisa kama ilivyotokea huko muheza,Mbali na hilo husababisha kushusha hadhi ya kanisa
Quote
 
 
0 #15 2011-08-12 12:09
Ni kichekesho sana. Lkn waandishi mnatuangusha sana na hizo title zenu!. Kusema amejifungua kanisani si sahihi. Kama alipelekwa hospitali na ndo akazalia huko then how comes unasema amejifungulia kanisani?.Andikeni kama mmesoma shule.Msilenge kuuza tu.
Quote
 
 
0 #14 2011-08-12 12:07
we Rwihura ni mtu wa ajabu sana dini yako ni ipi inayokubali watu waendelee na uzinifu eti tu wakitaka kufunga ndoa ndio waungame, hakuna ruhusa hiyo uzinifu ni kosa kubwa na tunatakiwa kuupiga vita si kuupigia debe kwa madai ya kuungama, sijaona mtu wa ajabu kama wewe
Quote
 
 
+2 #13 2011-08-12 10:17
Kulaumu Kanisa ni kwenda mbali sana. Bibi harusi na wapambe wake ndio walipaswa kuahirisha hiyo ndoa ili bibi arusi ajifungue kwanza. Tarehe ya ndoa inapangwa wiki hata mwezo kabla ya ndoa. Hivyo padri siyo kazi yake kujua kama huyu mwanamke yuko karibu kujigunua au vipi. Na ieleweke hakuna mahaali sheria inasema kuwa wana ndoa lazima wawe hawajutana kimwili eti ndi wafunge ndoa. Inawezekana hata wakawa wanakaa pamoja lakini kabla ya ndoa wanaungama.
Rwihura
Quote
 
 
0 #12 2011-08-12 10:14
u[NENO BAYA] mtupu..
Quote
 
 
+3 #11 2011-08-12 09:46
naamini kama ni katoliki ndoa ya aina hiyo haijafungwa! mwandishi kajiandikia tu kwani hana maadili ya uandishi. kichwa cha habari kajifungua kanisani, habari yenyewe kajifungulia hospitali teule ya muheza, kwa hiyo kajifungulia wapi? au kajifungua watoto wawili mmoja kanisani na mwingine hospitali? mwandishi mchochezi. akaombe kazi magazeti ya udaku atafanikiwa zaidi au mwananchi ni gazeti la udaku siku hizi?
Quote
 
 
-1 #10 2011-08-12 09:45
mambo ya sasa hivi makanisani ni ya hovyo sana tena aibu kubwa. Makanisa yamekuwa na rushwa na wanawanyenyekea sana wenye pesa na wanawabembeleza waumini wasieahame utafikiri benki. Zamani hakukuwa na mambo haya. Bi harusi mjamzito walitakiwa kuungama kwanza,hawakuru husiwa kuvaa nguo nyeupe, wala shela, wala kushika maua na ilikuwa ndoa ya kimya maana usafi halisi haukuwepo. Nasemea hasa Lutheran. siku hizi sasa, he he he. Na askofu anakuwa mbele hana wasiwasi hata tumbo la bibi harusi likimsu[NENO BAYA].Hata kama watasema si amri ya kwenye biblia lakini pia kanisa lisimamie sheria zake.Huyo ndafu ni Mungu alikasirika akamtupa huko. Na bado.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner