MwanzoContactsEmail
Home Habari Matukio ya kusisimua Polisi wapambana na wananchi, waua mmoja
BOOKMARK THIS PAGE
Polisi wapambana na wananchi, waua mmoja  Send to a friend
Sunday, 15 January 2012 21:23

Ahmed Makongo, Bunda
MWANAUME mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika vurugu za wananchi zilizotokea katika Kijiji cha Wegero, Musoma Vijijini.

Vuguru hizo zilitokana na wananchi kuwashtumu polisi kwamba wamemwachia mmoja wa watuhumiwa wa mauaji mwananchi mwenzao aliyemchomwa kisu.

Kamanda wa polisi mkoani Mara, Robert Boaz, alisema tukio hilo lilitokea juzi jioni katika Kijiji cha Wegero na kwamba aliyeuawa kwa kupigwa risasi ni Mgoyo Mgoyo, mkazi wa kijiji hicho.

Kamanda Boaz alisema a mtu huyo aliuawa kwa bahati mbaya katika jitihada za askari polisi kujihamini dhidi ya kundi kubwa la wananchi waliokuwa wakishambulia kwa mawe.

Alisema katika tukio hilo askari polisi walipofyatua risasi hewani na kwa bahati mbaya moja ilimpata mtu huyo na kupoteza maisha.

“Mtu huyo ameuawa kwa bahati mbaya katika jitihada za polisi kujihami kwa kufyatua risasi hewani. Zilikuwa vurugu kubwa maana wananchi walikuwa na jazba sana na walikuwa na silaha za jadi kama mawe ambayo waliyatumia kuwashambulia askari," alidai.

Alisema kuwa vurugu hizo zilizuka baada ya uvumi kwamba mwananchi mmoja anayeshikiliwa na polisi kwa tuhuma ya mauaji ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, aliyeuawa Desemba 26 mwaka jana kwa kumchoma na kisu ameachiwa huru, baada ya ndugu zao kuwaonga polisi.

Alisema kufuatia uvumi huo wananchi walikwenda nyumbani kwa ndugu wa mtuhumiwa na kubomoa nyumba zipatazo 12, na kuteketeza maghala ya chakula na mabanda ya mifugo kwa madai kuwa wao ndio walioonga pesa polisi ili kuwezesha ndugu yao kuachiwa.

Kamanda huyo alisema kufuatia vurugu hizo, uongozi wa Wilaya ya Musoma ulimtuma Ofisa Tarafa kwenda katika eneo la tukio, lakini alipofika wananchi walimfukuza, hatua iliyomlazisha kutoa taarifa polisi.

Alisema hata hivyo polisi walipokwenda katika kijiji hicho nao  walishambuliwa kwa mawe na kusababisha gari moja ya polisi kuvunjwa tata na vioo huku skari mmoja aiwa amejeruhiwa.

 “Kutokana na vurugu hizo polisi walilazimika kuondoka katika katika eneo wakiwa wamewachukuwa baadhi ya viongozi hao na kuwapeleka mahabusu," alisema.

Hili ni tukio la pili kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuteketeza nyumba za wananchi wenzao katika kipindi kisichozidi wiki moja.

Hivi karibuni wananachi wa Kijiji cha Mwibagi, Musoma Vijijini, waliziteketeza nyumba zaidi ya 15 za familia sita tofauti, wakazi wa kijiji hicho, wakiwatuhumu kuwa ni washirikina na majambazi.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #6 2012-01-17 00:01
siku hizi watu wanamabawa/?
Quote
 
 
0 #5 2012-01-16 16:04
Wananchi hawawaamini Polisi- walinda amani wetu wamepoteza sifa kutokana na vitendo aidha vya Rushwa, polisi hao hao kuhusika na vitendo vya ujambazi nk.
Ktk hali iliyopo njia pekee imebaki kwa wananchi ni kuchukua sheria mikinoni.
Quote
 
 
0 #4 2012-01-16 16:02
Hawa watu wa musoma ni wachezi kwani wao kila kitu wanachukilia hasira maana yake ni nini? kubobomoa nyumba ya mtu eti ni kuhisi kuwa ametoa pesa polisi, pia wana roho mbaya sana hawa jamaa wa musoma.. Wakuliya ata sura zao zinaonyesha roho mbaya.
Quote
 
 
0 #3 2012-01-16 15:58
Quoting mjomba:
Kwani hewani kunakaa watu!

Ahsante sana kaka kwa kuwauliza hilo swali. kama kawaida yao watajibu kuwa wataunda tume ya kuchunguza then wanapotezea kama kawaida yao.
Quote
 
 
0 #2 2012-01-16 14:18
hawa ndugu zetu haitakiwi kuwadanganya
niwatu wanao hitaji ukweli minimekaa buhemba mining nimekaa nyamongo hakuna shida ukiwa mkweli utaishi raha msitarehe
Quote
 
 
0 #1 2012-01-16 06:49
Kwani hewani kunakaa watu!
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner