MwanzoContactsEmail
Home Habari Matukio ya kusisimua Polisi wauawa wanne wakidaiwa majambazi
BOOKMARK THIS PAGE
Polisi wauawa wanne wakidaiwa majambazi  Send to a friend
Tuesday, 24 January 2012 20:39

Suzy Butondo, Shinyanga
WATU wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuwa kwenye pambano na polisi Kijiji cha Nyambula, wilayani Kahama, mkoani hapa wakidaiwa kujiandaa kufanya ujambazi kwa wafanyabiashara eneo la Kakola na mgodi wa Bulyanhulu.
Wanadaiwa walikuwa na silaha za kivita na mapanga, walikuwa wakisubiri usafiri  wenzao, lakini kabla polisi walipata taarifa kwa raia mwema  kuhusu uwapo wa majambazi saba wenye silaha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athuman, alisema majambazi hao waliuawa saa 4:30 usiku na kwamba, baada ya kupata taarifa polisi waliandaa mtego kwa kuwapelekea majambazi hao usafiri eneo walikuwa.

Diwani alisema baada ya kufika eneo hilo walikuta ishara ya mfuko wa plastiki uliowekwa jiwe juu yake na majambazi hao waligundua kuwa gari hilo lilikuwa  linawasubiri wao, ndipo walipoanza mashambulizi dhidi ya askari ambao nao walianza kujibu mapigo na kuua waane kati ya saba.

 Hata hivyo, Diwani alisema majambazi watatu walifanikiwa kukimbilia porini  na eneo hilo zilipatikana silaha mbili aina ya SMG namba AF364750 na risasi 22 na namba 0801 ikiwa na risasi 25. Risas nyingine 132 zilikutwa kwenye mfuko wa plastiki.

Alisema baada ya kupekuliwa walikutwa na simu tatu, fedha za Burundi Faranga 10,000 na Sh2,000. Pia, waliokota kitambulisho cha uraia wa Burundi cha Ndikumana Erick.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #2 2012-02-03 15:13
2nawaomba police waendelee na kazi yao nzuri kwani hawa raia wakigen wana2letea vitendo vya kinyama! Kwenye nchi ye2 ya amani.
Quote
 
 
+1 #1 2012-01-25 14:28
kweli kahama kuna hali y akuogopesha.inabidi wnanchi washirikiane na polisi ili kuweza kuwadhibiti hao majambazi.ila huko kahama watu wengi au wakigoma wengi ndio huchukulia treni za kwenda kwao ndo maana hta wnapat amwanya wa kufanya uhalifu huo .na pia hii inachangiwa na wakimbizi wengi wa burundi kuishi kigoma....ulinzi uwepo jamani
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner