MwanzoContactsEmail
Home Habari Matukio ya kusisimua Mfanya usafi akamatwa akimlawiti mtoto msikitini
BOOKMARK THIS PAGE
Mfanya usafi akamatwa akimlawiti mtoto msikitini  Send to a friend
Tuesday, 24 January 2012 20:40

Hamisi Mwesi, Dodoma
POLISI mkoa hapa  inamshikilia mkazi wa Bahi Road, Manispaa ya Dodoma, kwa tuhuma za kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka tisa baada ya kumpa Sh500 ili kumfichia siri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen, alisema mtuhumiwa huyo ambaye ni mfanya usafi wa Msikiti wa Ghazal uliopo eneo la Majengo, alitenda kosa hilo juzi saa 12:00 jioni.
 
Stephen alisema baada ya polisi kupewa taarifa na wananchi wa eneo hilo, walifika msikitini hapo na kumkamata mtuhumiwa akiwa ndani ya choo cha wanawake alipokuwa akifanyia mtoto kitendo hicho cha kinyama.

“Polisi walijulishwa na wananchi waliokuwapo eneo hilo kwamba mtuhumiwa alimuingiza mtoto huyo kwenye choo cha wanawake na kujifungia ndani, watu waliokuwa jirani na eneo hilo walifuatilia kwa makini ndipo waliposhuhudia mtuhumiwa akimlawiti mtoto huyo na kutoa taarifa polisi,” alisema Stephen.

Alisema mtoto huyo amelazwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kutokana na maumivu, kutokana na kitendo hicho na hali yake inaendelea vizuri na uchunguzi juu ya afya yake unafanyika kubaini athari zaidi.

Alisema mama mzazi wa mtoto huyo, alimg’ata sikio la kulia mtuhumiwa huyo kwa hasira na kunyofoka nusu ya sikio lake na kwamba, hivi sasa wanashikiliwa.

Inadaiwa mtuhumiwa amekuwa na tabia hiyo muda mrefu na waumini wa msikiti huo waliwahi kumuonya, baada ya kutiliwa shaka kuhusu kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo hawakuwa na ushahidi, ndipo walipoamua kuanza upelelezi dhidi yake.

“Waumini walishamshtukia mtuhumiwa, wakaanza kufuatilia nyendo zake kwani yeye muda mwingi hukaa msikitini kwa ajili ya kufanya usafi, wakati mwingine kutoa adhana kwa ajili ya swala, leo (juzi) amenaswa na mtego baada ya kumtanguliza mtoto choo cha wanawake na yeye kumfuata,” alisema mmoja wa waumini wa msikiti huo.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #12 2012-03-05 11:25
huyo hafai kabisa tabia mbaya
Quote
 
 
0 #11 2012-02-14 08:47
Inasikitisha sana jaman, sasa ina mana gani kukaa ndani ya nyumba ya Mungu.
Quote
 
 
-1 #10 2012-02-06 22:26
2natakiwa kutubu na kudumu katika maombi tumwamini BWANA YESU kwa kuwa yeye anayaweza yote.
Quote
 
 
0 #9 2012-02-03 09:26
"Si wote wajiitao kuwa ni watumishi wa MUNGU,kana kwamba ni kweli wengine ni watumishi wa Shetani.Mtu kama huyo atengwe na kusimamishwa huduma.Hata huku kwetu mchungaji amembaka binti wa miaka 16.
Quote
 
 
0 #8 2012-01-26 06:38
Hakuna binadamu aliyekamilika...na hayo ni mapungufu kawaida...hayausiani na imani ya mtu.....
Quote
 
 
0 #7 2012-01-25 14:49
dah! kweli dunka imeisha hadi muadhini anakula kiboga anapaswa kunyongwa na si kupigwa bakora hadi kufa
Quote
 
 
+2 #6 2012-01-25 13:42
Sasa huyo ndio anayetakiwa kuitwa kafiri, sio hao wengine mnaowasingizia ambao wengi wao ni ni waadilifu sana kuliko nyote mnaolitamka neno kafiri kiurahisi sana juu ya wenzenu!
Quote
 
 
+1 #5 2012-01-25 13:01
huyo mshenzi wa tabia hafai katika jamii inabidi apigwe mawe mpaka afe kama ilivyo sheria ya kiislamu manake kadhalilisha mskiti na hasa waumini wa dini ya kiislamu .
Quote
 
 
0 #4 2012-01-25 12:47
huyo mshenzi acha afie jela hafai kukaa na jamii hasa ikitiliwa maanani yeye anafanya kazi katika nyumba tukufu ,mi nafikiri itumike adhabu ya kiislam apigwe mawe mpaka afe ndo adhabu anayostahili kwa kosa hilo.
Quote
 
 
0 #3 2012-01-25 10:29
mama alipashwa kung'ta nyeti sio sikio!!!!! ang'ofoke nayo!
Quote
 
 
+1 #2 2012-01-25 09:12
angemng'ata pua kabisa mshenzi huyo. na hao waumini wanatakiwa wajifunze siku nyingine mtu anayefanya kazi sehemu takatifu akihisiwa tu basi anatakiwa asimamishwe
Quote
 
 
+1 #1 2012-01-25 08:46
mwadhini huyo! maustadh wetu hao!
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner