
| Mkapa apokelewa kwa kushindo Songea | Send to a friend |
| Thursday, 02 September 2010 22:21 |
|
MAMIA ya wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, jana walilazimika kuacha shughuli zao kumlaki Rais mstaafu Benjamin Mkapa, huku wakimshangilia na wengine wakiimba nyimbo za kumpongeza. Katika tukio hilo, baadhi ya wananchi walishika mabango yaliyomsifu kiongozi huyo na mengine ya kumbuka kwa mazuri na maendeleo wananchi akiwa madarakani. Mkapa aliwasili mjini Songea saa 11:57 jana akiwa na mkewe, Anna Mkapa wakitokea jijini Dar es Salaam, kwa kutumia ndege ya kukodi. Katika uwanja wa ndege wa Songea, kiongozi huyo wa serikali ya awamu ya tatu, alipokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM, serikali wa madhehebu ya na wananchi kwa jumla. Mkapa yupo mkoani Ruvuma kwa mwaliko wa Kanisa Katoliki, ambalo leo linaadhimisha Jubilei ya Seminari ya Lukonde na anatarajiwa kuondoka kesho. Katika uwanja wa ndege, Mkapa alikagua vikundi mbalimbali vya ngoma na burudani na muda wote alionekana akiwa anatabasamu kutokana na kuguswa na ujumbe wa vikundi vilivyokuwa vikitumbuiza na kumpongeza. Walisema katika uongozi wake, Mkapa alifanya mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, shule za msingi, sekondari, Daraja la Mkapa na uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu. " Karibu mkombozi wa wanyonge mkoani Ruvuma ujio wako umetukumbusha mazuri uliyotufanyia, Mungu akujalie afya njema daima tutakukumbuka," lilisomeka moja ya mabongo Akitoa maoni yake kuhusu kiongozxi huyo mstaafu, Ashuara Kazumari alisema Mkapa alikuwa mchapakazi, mzalendo na kiongozi mwenye busara, aliyesaidia kuharakisha maendeleo ya wananchi. Kwa upande wake, Boniface Mrema alisema amefurahishwa na ujio wa kiongozi huyo na kwamba umewakumbusha wananchi wa Ruvuma mambo mengi aliyoyafanya wakati wa uongozi wake . |













