JPM atoa msamaha kwa wafungwa 3,000

Muktasari:

  • Rais anatoa msamaha huo kwa mujibu wa ibara ya 45(1) (d) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,319 katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo.

Taarifa iliyotolewa leo Aprili 26 na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira, imesema, wafungwa 585 wataachiwa huru kuanzia leo, huku wengine 2,734 wakipunguziwa kifungo na hivyo wataendelea kubaki gerezani hadi watakapomaliza sehemu ya kifungo kilichobaki. 

Rais anatoa msamaha huo kwa mujibu wa ibara ya 45(1) (d) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 “Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Msamaha mwingine unahusu wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama vile ukimwi, kifua kikuu na saratani.

Jenerali Rwegasira amesema wafungwa hao ni lazima wathibitishwe na jopo la waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Mganga Mkuu wa Wilaya.

Kundi la tatu linahusu wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi.

Jenerali Rwegasira amesema umri huo uthibitishwe na jopo la waganga.

“Pia kuna wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili, na ulemavu huo uthibitishwe