|
Fredy Azzah RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali imebuni mpango maalumu wa kutumia mkongo wa mawasiliano, ili kukabiliana na upungufu wa walimu katika shule za sekondari nchini.Katika kufanikisha jambo hilo, shule zote za sekondari zitaunganishwa katika mtandao huo ambao utawawezesha mwalimu mmoja kufundisha shule hizo wakati mmoja. Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Januari mwaka 2006 na kutoa maagizo ya kuboresha elimu kwa miaka mitano ijayo.
"Pamoja na kuwa tuna tatizo la upungufu wa walimu kwa jumla, hali ni mbaya sana kwa walimu wa sayansi, mpaka sasa kuna upungufu wa walimu 34,000 na sisi kwa mwaka uwezo wetu ni kuzalisha walimu 10,000," alisema Rais Kikwete.
Alisema ili kukabiliana na tatizo hilo, serikali itaziunganisha shule za serikali katika mkonga wa taifa wakati ikiendelea pia kuzalisha walimu kadri itakavyoweza."Kutokana na idadi ya walimu wanaosoma, tatizo la walimu litaweza kwisha baada ya miaka mitatu, lakini sasa pamoja na walimu 10,000 kumaliza masomo yao kwa mwaka, unaweza kukuta bado tuna upungufu wa walimu 40,0000 kwa mwaka," alisema
"Tukiziunganisha shule zetu kwenye mkongo wa taifa ambao mpaka kufikia Juni mwaka huu utakuwa umekamilika, mwalimu mmoja akiwa hapa, anaweza kufundisha wanafunzi wa kemia nchi nzima kwa wakati mmoja." alisisitiza.
Alisema mpango huo ukifanikiwa mwalimu atakaye kuwa yupo kwenye darasa la shule husika, kazi yake itakuwa ni kusimamia wanafunzi kufanya mazoezi na yatakayotolewa na mwalimu aliyekuwa akifundisha kwa njia ya mtandano na kusahihisha kazi zao.
Alieleza kuwa, tayari serikali imeshafanya mazungumzo na kampuni moja ya Kimarekani ambayo itasaidia katika teknolojia hiyo."Wameshanionyesha jinsi tutakavyofanya kwenye maeneo ambayo yana umeme na hata yale yasiyokuwa na umeme," alisema Rais Rais pia aliitaka wizara kuweka bayana mipango yake kuhusu namna ya kuinua ubora wa elimu.
|
Comments
Alishabikia sheria ya Uchaguzi kumbe ilikuwa na kasoro nyingi tena za wazi.
Awamu ya nne ni vichekesho vitupu
Maabara za kufanyia mazoezi kwa vitendo zipo??
Nina uhakika huu mpango ni ghali sana kuliko kuajiri walimu, na ni mgumu kuutekeleza katika mazingira ya Tanzania bila maandalizi ya muda mrefu.
Vyuo vyetu vikuu havina hata hayo mawasililano ya internet ya uhakika leo Jk anakuja na hadithi ya kuwa na kutumia mkongo wa mawasiliano kufundishia shule za sekondari, huu si Uwe ndawa zimu jamani??
A visonary leader will always set realistic goals, after he has done feasibility studies...hapa mimi naona ni usanii mwingine tena wa serikali ya Jk
Hakuna siku nimekatishwa tamaa lakini nikacheka kama leo kuhusu habari hii. Sijui kama uwezo wa ki-miundo mbinu uko juu kiasi hicho. Na sijui kama mkwere anajua vizuri analolisema. Si vizuri kudharau mamlaka ya juu kiasi hiki lakini mtu unajikuta huna chaguo.
Hahahahahahahhh h!!!
Did you know that one day you will be in the position to use computer as you do?! What is so special for a teacher to stand before teaching lab and teach! By the way, kama aina hii ya Elimu in question haijawahi na wala haitolewi popote hapa duniani, I can understand. If you please, revisit your statistic.
1) Pikipiki (Bajaj ambulance) kwa wajawazito na wagonjwa
2) Elimu Mkongo kwa shule zote za sekondari
3) Kununua/kukodi mitambo ya DOWANS kupunguza makali ya umeme
4) Kuzuia maandamano sababu yanaleta umasikini na kuzidisha uhalifu
5)Mawaziri na watendaji wakuu wa Serikali kupingana hadharani
Kama hii ndio miundombinu, Kweli tumeliwa!!!!!!! !
1. Wawekeni walimu wenye uzoefu watengeneze syllabus yenye kuendana na dunia ya millenia ya tatu.
2. Ongezeni mishahara ya walimu. Hiyo mishahara mikubwa wanayopewa wabunge, mawaziri na watendaji wa serikali, ipunguzwe na walimmu waongezewe mishahara yao na kuondolewa kero mbali mbali. Hao wabunge, mawaziri au watendaji bila ya kupata walimu wasingelikuwa katika nafasi walizonazo leo hii na kupata mafanikio waliyo nayo. walimu waongezewe hali bora ya mishahara. Walimu wakipata motisha watafundisha kwa bidii, hawatahangaika kukatikza masomo kwa ajili ya kwenda kujitafutia njia nyingine za mapato, watakuwa na muda wa kutosha kuwafuatilia wanafunzi. Kama mwalimu kwenda kupokea vijisenti vya mshahara wake anazungushwazun gushwa mara huku mara kule, atapata muda gani wa kufundisha? MISHAHARA YA SASA YA WALIMU IONGEZWE MARA TATU ZAIDI. Hivyo walimu watapata motisha.
3. Ondoeni siasa katika sekta nyeti. Wizara kama ile ya elimu, ya afya, ya ujenzi au fedha, inahitaji watendaji wake wakuu kuanzia mawaziri wake kuwa watu wenye uzoefu na usanifu na sekta wanayopewa. Kama sekta ya elimu wakipewa watu ambao hawajui matatizo ya shule, ya wanafunzi, kero za walimu, itakuwa vigumu kwake kutoa sera muafaka za kuboresha sekta hiyo na watendaji wake.
4. tatizo la elimu halitatuliki kwa mikonga, kwani kama ni hivyo wanafunzi wanaweza kubaki nyumbani na kujisomea. Njia za kisasa za mawasiliano zinahitajika kufundishwa na kutumika, lakini haziwezi kum- substitute mwalimu hai. ni njia mbadala lakini haziwezi kumtoa nje mwalimu nje ya ulingo wake. Njia hiyo yaweza kutumika katika elimu za juu za vyuo, lakini kwa ngazi ya sekondari, elimu ni pamoja na maisha ya pamoja, ya kuelimishana, ya kujifunza "ELIMU" na kujenga hoja nyoofu... hapa hakuna jinsi: unahitaji mwalimu, dawati na wenzako. siyo internet. Pia nina wasiwasi na njia hiyo kwani inaua sana mawasiliano ya ki-utu kama ilivyo katika nchi zilizoendelea.
5. Pia tumeanzisha vituo vya elimu vingi mno na hata watu binafsi wameanzisha vituo vya elimu vingi, lakini hawakuanzisha SHULE. shule zina misingi yake... walimu wasanii walioandaliwa vizuri, majengo ya kutosha, maabara ya majaribio, maeneo makubwa kwa ajili ya recreational activities, nyenzo na facilities nyingine. Shule nyingi za kata ni vituo vya elimu au madarasa ya tuition lakini hazina hadhi ya shule. utakuta shule ina walimu 5...hata ukiwa na form one tu idadi hiyo haitoshelezi hata kidogo. Tuanzishe shule, na siyo vituo vya elimu
"Mtu anayefanya jambo lilelile kwa njia ileile akitegemea mabadiliko" sasa kutokana na kufeli mwaka jana je nini tofauti kimefanyika ili mwaka huu uwe tofauti? au tutegemee mtihani rahisi kupita kiasi ili kila aliyeko kidato cha nne mwaka huu afaulu? TANZANIA kazi tunayo..
maana, rais kanidharau na kuniona sina uwezo hata wakufikiri kwamba hiyo ahadi haitaweza tekelezeka ndani ya mika 200 ijayo. nakubari 80% ya shule za serikali zipo vijijini. Je, umeme ukikatika sehemu anayo fundishia huyo mwalimu?.
Rais Kiwete ni bora kipindi kile ulikaa kimya kabisaaaaa. Acha kuongea na kutoa ahadi kama hizi. kaa tu kimya, unazidisha hasira zangu, na si mimi tu.
ungetoa ahadi ya kuboresha vyuo vya walimu vilivyopo na kujenga vingine vingi ili kuwepo na uwezekano wa kuvuna walimu zaidi ya 10,000 kwa mwaka. hapo ningekuelewa.