MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Serikali yawapiga marufuku waganga
BOOKMARK THIS PAGE
Serikali yawapiga marufuku waganga  Send to a friend
Thursday, 24 March 2011 21:21

Anthony Mayunga, Musoma

WAGANGA wa tiba za jadi nchini ,wanatakiwa kuacha mara moja kudanganya watu kuwa wanatibu magonjwa kama kifua kikuu, kisukari na Ukimwi kwa kuwa sheria haziwataki kujitangazana badala yake wanapaswa kutangazwa na wanaopata tiba na kupona.

Onyo hilo kali limekuja wakati maelefu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa wanaendelea kumiminika katika Kijiji cha Samunge kupata tiba kutoka kwa Mmchungaji mstaafu
Ambilikile Mwasapile.

Mchungaji huyo amekuwa akitibu  magonjwa sugu yakiwemo kifua kikuu, kisukari, Ukimwi, degedege na shinikizo la damu.Onyo dhidi ya waganga, lilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Lucy Nkya, katika hotuba yake kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kifua kikuu Duniani.

yaliyofanyika  kitaifa mkoani Mara.
Alisema kuenea ugonjwa wa kifua kikuu unaenea kwa kasi kwa sababu  wananchi wanakubali kudanganywa na waganga hao.

“Nasema kuanzia sasa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji, kuwadanganya wagonjwa kuwa wanatibu magonjwa kama hayo, maana mnadanganya watu na wanazidi kufa. Hatutaruhusu tena mchezo huo, narudia ni marufuku, tiba halisi inatolewa hospitalini si kwingineko," alisema Naibu Waziri.

Alisema waganga wazuri hawajitangazi na kwamba wanaopaswa kujitangaza ni wafanyabiashara tu  ambao kazi yao kudanganya watu kwa kutumia matangazo mazuri mazuri.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo hakugusia tiba inayotolewa na Mchungaji Mwasapile, ambayo watu mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, wamewahi kuitumkia.

Akizungumzia mikakati ya serikali kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu, alisema wizara imeanza kusambaza aina mpya ya darubini za kisasa za LED, zenye uwezo mkubwa zaidi wa  kugundua vimelea vya kifua kikuu katika makohozi.

“Hadi kufikioa mwisho wa mwaka huu, asilimia 95 ya hospitali zote za wilaya, zitapata darubini hizi mpya na ifikapo mwishoni mwa 2012 hospitali zote zikiwemo za mashirika ya dini zitakuwa zimepata, vifaa vipya vya
kuoteshea vimelea vya kifua kikuu,”alisema na kuongeza.

Alisema  vifaa hivyo vitafungwa katika maabara za Hospitali za Muhimbili, Mbeya, Bugando na Kibong’oto.

Alikiri kuwa wizara hiyo inakabiliwa na upungufu wa wataalam wakiwemo mafundi sanifu wa maabara na uelewa mdogo wa jamii  kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #4 2011-03-26 05:52
Je mganga huyo atakuwa tayari kuniozesha binti yake baada ya kunitibu ukimwi kwa hiyo dawa? Pia je serikali itachukua hatua gani iwapo watu waliotibiwa hawakupona baada ya tabu zote walizopata katika usafiri kwenda kwake mganga272yp?
Quote
 
 
+1 #3 2011-03-25 12:03
ya napia viongozi muwe na huruma nawananchi wenu,kwani mengi nyie wenyewe niwataalamu,nam metokea ktk idara mbali mbali km wewe ni DR nawajua mengi,naomba muwe watekelezaji/wafuatiliaji wa hayo mnayoyaongelea isiwe tu kupokea per diem na kuendelea navikao vingine.Na nibora mkafika izo sehemu husika tukasikia mnayoyatekeleza ,chukueni mfano wa Vl Putin Na Medyedyvo.Nakutakia kazi njema Mh Naibu Waziri.Pia wekeni mazingira mazuri na malipo mazuri kwa wafanyakazi wa afya ila wataalamu wa afya tusiwe wenyekuacha taaluma zakiafya nakuuza magazeti hatimayake kunakua na upungufu wawatu husika
Quote
 
 
+1 #2 2011-03-25 11:57
Nyongeza nikwamba pia kkutokana naongezeko la maambukizo ya Maambukizi ya VVU/UKIMWI kifua huongezeka.
Namadhara makubwa kwa watu wanaoacha kutumia dawa za kutibu Kifua kikuu au dawa zakupunguza makali ya UKIMWI ni Usugu.(drug resistence)
Kwa upande mwingine wenda nivyema serikali kukaa nawatu husika(hao waganga au wataalamu wanaosema wanatibu magonjwa husika)kuwaelim isha matatizo husika nakufanyia utafiti izo tiba.Na uwakika kabisa ilo lawezekana,wend a watapunguza kasi yakujitangaza.Psychology ya mgonjwa wowote mw magonjwa sugu ni sawa ya mtoto mdogo,anakua "naive"mno,kiasi kudanganyika niwepesi amini usiamini
Quote
 
 
0 #1 2011-03-25 11:39
siasa na ndiyo umeshamliza hapo. ufuatiriaji zero. nafikiri ni bora kusiwe na utaratibu wa kuhutubia wananchi wakati wa kuadhimisha hizi siku. maana mnaongea mengi na kukataza mengi halafu hakuna ufuatiriaji. mkishazungumza kwenye majukwaa mkishuka mnasini posho zenu mnatia katika mifuko na kurudi ofisini kuendelea na utatatibu wetu wa kila siku watanzania " majungu"
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner