
| Wanaomuiga Babu wazidi kuongezeka | Send to a friend |
| Monday, 04 April 2011 22:08 |
|
WIMBI la waganga wanaomuiga Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wa Samunge Loliondo, Ambilikile Mwasapile, limezidi kuongezeka baada ya mganga mwingine mkoani Iringa, kuibuka na kudai kuwa ana tiba ya aina hiyo. Mganga huyo, ametajitambulisha kuwa ni Antony Mwandulami kutoka katika Kijiji cha Wangama, wilayani Njombe.Mwandulami alidai kuwa amekuwa akitumia mti kama ule unaotumiwa na Mchungaji Mwaisapila, kutibu magonjwa sugu.Alidai kuwa tayari imepita wiki moja tangu aanze kutoa tiba hiyo na kwamba, watu wameanza kujaa nyumbani kwake. Kwa mujibu wa mganga huyo, tiba yake inagharimu Sh2,000 kulingana na ugonjwa wa mteja wake."Niliangalia kwenye TV, nikagundua kuwa mti anaoutumia babu hata mimi nilikuwa nikiutumia siku nyingi lakini sikuwa napata mafanikio kwa sababu nilikuwa nikichanganya dawa nyingi. Nilipogundua babu anachemsha mti huo tu, nikaiga na sasa nimeona mafanikio," alisema Mwandulami. Alisema watoto wa chini ya umri wa miaka 14, amekuwa akiwapa dawa hiyo bure na kwamba, yeye hajaoteshwa kama ambavyo wengine wamekuwa wakidai.“Huu mti nilikuwa nikiujua siku nyingi, nilionyeshwa na mizimu isipokuwa tatizo ndo hilo la kutochemsha ukiwa peke yake," alisisitiza. Wakati mganga huyo akiwa tayari ameanza kutoa tiba hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Utendaji ya Chama cha Waganga wa Jadi mkoani Iringa, Pangael Msekwa, aliwataja wananchi kujihadhari na wimbi la waganga wanaojitokeza kutibu magonjwa sugu.Alisema kuna uwezekano kuwa waganga hao wanaomuigiza babu wa Lilondo ni matapeli. |
















Comments
Mwisho wa siku itajulikana tu kwamba wote ni wezi. Wanatumia U[NENO BAYA] wa Watanzania kuwaibia na kuwasahaulisha matatizo yao ya msingi.