MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Polisi, mahakama zazidi kutajwa kwa rushwa
BOOKMARK THIS PAGE
Polisi, mahakama zazidi kutajwa kwa rushwa  Send to a friend
Wednesday, 25 May 2011 21:54

Minael Msuya

IDARA za POLISI na Mahakama zimetajwa tena kuwa  ni taasisi sugu zinazoongoza kwa kudai rushwa nchini.Kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHCR) katika taarifa yake imezitaja idara hizo kwamba ndizo kinara kwa kudai rushwa.
Hivi karibuni, Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa Takukuru)  nayo ilizitaja idara  hizo kwamba ndizo zilizo mstari wa mbele kudai rushwa nchini.

Ripoti ya mwaka 2010 ya LHCR iliyofanywa katika mikoa 26 nchini na kuhoji watu zaidi ya 5,000, ilibainisha kuwa  polisi inaongoza kwa asilimia 65.1 huku Mahakama ikifuatia ikiwa na asilimia 56.4. Akisoma ripoti hiyo,  Mwanasheria wa LHCR, Pasience Mlowe alisema polisi na mahakama  zinaongoza kwa rushwa na matumizi mabaya ya ofisi na kwamba zinashika nafasi ya 10 kwa Afrika Mashariki.

 “Utafiti wa LHCR ulibaini kuwa polisi na mahakama ni taasisi sugu zinazoongoza kwa rushwa na zinashika nafasi ya 10 kwa Afrika Mashariki,” alisema Mlowe.

Alisema  Mamlaka ya  Mapato Tanzania  (TRA) nayo inafuatia  kwa asilimia 37.8  na kwamba inaendelea kushuka kiwango kila siku ikilinganishwa na 2009 ambapo ilikuwa katika nafasi ya tano. “Hali hii inayonyesha ni jinsi gani baadhi ya watu walivyozitelekeza sheria na haki za binadamu, wananchi wengi wanataabika usiku na mchana, lakini hawapati haki zao stahiki, tunaomba marekebisho ya vifungu vya sheria yafanyiwe kazi ili haki ya binadamu iweze kupatikana,”alisema.

 Mlowe alisema, matatizo hayo ya taasisi hizo nyeti za serikali yanachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha uchumi wa nchi na kwamba serikali inatakiwa kusimamia sheria muhimu.  Kwa upande wake ,Mtafiti na Mwanasheria wa LHCR, Onesmo Olengurumwa alieleza kuwa, utafiti huo ulibaini kuwa mauaji ya raia wengi yanasababishwa na vyombo vya dola kutokana na wao kujichukulia sheria mikononi.

 “Vifo vya watu 52 vilivyotokea mwaka 2010 vilisababishwa na walinzi wa kampuni mbalimbali na polisi kwa kujichukulia sheria mikononi  badala ya kutumia sheria inayowaongoza,”alisema Olengurumwa na kuongeza:  ”Mfano mzuri ni wananchi wanaoishi kando ya Mgodi wa North Mara kule Tarime wanauawa bila sababu  na ukichunguza utakuta sheria za mgodi, walinzi wa kampuni  ndio wanaopaswa kulinda eneo lote sasa serikali inaingiliaje huko,”alisema.  

Alisema mauaji ya watu yaliyotokana na mgodi huo, serikali haiwezi kujitetea kwa lolote na kwamba utetezi wake ni wakisiasa.  Alisema serikali ikisimamia tume ya sheria na haki za binadamu nchi itaweza kuondokana na changamoto za ukiukwaji wa haki hizo zinazoikabili.  


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #1 2011-05-26 18:02
Ukifika polisi kuleta dai lako unaambiwa toa hela ya kununuli kalamu na karatasi ukishatoa unaambiwa hebu tuchemshe matumbo yetu maana bado asubuhi baadayeunaambiw a lete hela tuweke mafuta tukamkamate mtuhumiwa.Uhamiaji ukifika utakutana na bango Bribe free zone area ukisogea mbele hata kama ni mtanzania au sio mtanzania utaambiwa toa sh flani tukupe passpot ya mda au nenda mahakamani ukatafute affidavit ya babu mzaa babu yako.Ukifika mahakamani utaambiwa itabidi uende kijiji mtafute hata rafiki wa babu mzaa babu yako waliyekua naye Ukweli atakuwa hayupo maana atakuwa lazima amekufa.Basi hapo ujue unaombwa hela kidogo
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner