MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Utafiti: Waliopata kikombe cha Babu wengi wamepona
BOOKMARK THIS PAGE
Utafiti: Waliopata kikombe cha Babu wengi wamepona  Send to a friend
Wednesday, 03 August 2011 22:59

Leon Bahati
ASILIMIA 78 ya watu waliotibiwa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapila, walipona magonjwa yao.

Hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Synovate kuanzia Mei 2 hadi 19, mwaka huu na kuwahoji watu 1,994 wenye umri zaidi ya miaka 18 maeneo mbalimbali nchini.Utafiti huo uliotolewa na Synovate kwa gazeti hili jana, unaeleza kuwa ni asilimia saba waliosema hawakupona wakati asilimia 15 walisema hawajui.

“Asilimia 78 ya waliotibiwa kwa kikombe cha Babu wa Loliondo, walisema wamepona magonjwa yaliyokuwa yanawakabili,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo ya utafiti.

Utafiti wa Synovate umekuja wakati ambapo utafiti wa awali uliofanywa na serikali juu ya dawa hiyo ya Babu kuinyesha kuwa ina uwezo wa kutibu magonjwa sugu kama vile kisukari, saratani, moyo na Ukimwi.

Serikali ilisema bado inaendelea na utafiti zaidi juu ya dawa hiyo, ambao unaweza kuchukua muda wa hadi miaka mitatu ikizingatia kuwachunguza waliotibiwa na kiwango cha dozi, kulingana na aina ya ugonjwa.
Ripoti ya Synovate inaonyesha ingawa ni watu wengi wanaotamani kuponyeshwa dawa ya Babu, ni Watanzania wachache wenye uwezo wa kumudu gharama za kwenda Loliondo.

Asilimia 83 walisema ni vigumu kupata dawa ya mchungaji huyo maarufu kama Kikombe, huku asilimia 17 wakaonyesha hakuna tatizo la kumfikia.Hata hivyo, kati ya waliokwenda asilimia 25 hawakuwa tayari kutaja magonjwa waliyokwenda kutibiwa, wakati asilimia 24 walisema ni kisukari.

Magonjwa mengine na asilimia ya watu walioenda kutibiwa kwenye mabano ni moyo (22), Ukimwi (13), saratani (12), vidonda vya tumbo (7), pumu (5), magonjwa ya ngozi (4), maumivu ya miguu (4), kifua kikuu (3), maumivu ya tumbo (3), maumivu ya uti wa mgongo (2), maumivu ya kifua (2), macho (1) na waliokwenda bila tatizo maalumu (3).

Mchungaji Masapila alijijenga umaarufu mkubwa kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu baada ya watu kutoka sehemu mbalimbali nchini na nchi jirani kujitokeza kwa wingi kupata tiba hiyo.
Hali hiyo ilisababisha baadhi ya ndugu kuwachukuwa wagonjwa wao waliolazwa hospitalini kuelekea kwa Babu, yapata kilomita 400 kutoka mjini Arusha.

Misururu mirefu ya magari ilijipanga kwenda kwa babu na kufanya watu kutumia hadi siku saba kupanga foleni ya kupata dawa.

Pia, utafiti wa Synovate ulizingatia kuwa kulikuwa na waganga wa jadi waliojitokeza kutoa tiba sawa na Masapila, lakini licha ya hali hiyo, asilimia 60 walikiamini Kikombe cha Babu.

Wengine waliojitokeza na asilimia za kuaminika kwa watu kwenye mabano ni Dogo Jafferi wa Mbeya (9), Magret maarufu kama Bibi wa Tabora (8), Subira Ali (4), Majimarefu (2), Sinkala wa Mbuyuni (2) na babu wa Moma Mtwara (2). 


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
+1 #27 2011-08-06 19:44
Mimi binafsi mwanangu amepona akikabiliwa na tatizo la kansa, ambyo pia ilimuua mke wangu na zilikuwa zinafanana, kwa hakika hao ambao mpaka wanakasirika kuhusiana na tiba ya Mchungaji mnanishangaza na wengi wenu mnaharibikiwa kutokana na kutaka kushindana na nguvu usizozifahamu hata kama huziamini. na maosema ovyo hamjapata matatizo hasa ya ugonjwa
Quote
 
 
0 #26 2011-08-05 06:41
Quoting Kijo:
Quoting mdau:
Synovate mlitumia maabara gani kwenye utafiti wenu? Isije ikawa mnatuletea mambo ya placebo effect.


Mvivu wa kusoma habari kwa makini,unakurup uka, habari inasema waliuliza watu waliotumia dawa wewe unaleta habari za maabara, mfuasi wa kakobe nini?

Duh! ulishaona wapi mtu anajua kuwa kapona kwa kujitazama? KJ unaonesha haujui lolote kuhusiana na mwili wa mwanadamu na maradhi wewe unadhani unalitetea neno la BWANA kumbe unawapoteza watu sasa subiri hasira za bwana zije zikushukie
Quote
 
 
0 #25 2011-08-05 06:28
Quoting Kijo:
Quoting the MAn:
teh teh wanasema wamepona wamepona ugonjwa gani? kwa kipimo kipi nyie wauwaji wakubwa mbona hamsemi kuhusiana na watu lukuki waliokufa baada ya kunywa dawa hiyo feki na kujidanganya kuwa wamepona na kuachana na matibabu ya hospitali waliyo kuwa wanayapata? Mie nadhani mna kampeni maalum ya kukarudisha hako Kazee kwenye chati


Tatizo lako mvivu wa kusoma habari kwa makini,unakurup uka tu!!!

mie naona weye ni mvivu hata wa kufikiria au unafanya kazi na hao M A bazazi hebu eleza hicho cha msingi ulichokisoma kwa makini? Halafu nani alikuambia kuwa ili kujua kama hicho kikombe kinatibu unahitaji kusoma magazeti itś like 1+1 sasa we subiri na imani za upofu
Quote
 
 
+1 #24 2011-08-04 18:28
synovate wametumia approach ya "ANKETA".Siyo necessarilly lab tech.
ANKETA ni mojawapo ya applicable methodologies maalumu zinazotumika....na ni sahihi kabisa...
msiwakatishe watu bure kuhusu hii tiba poa!!Jamani tuzidi kupata kikombe cha babu...viva synovate....viva KIKOMBE CHA LOLIONDO KWA BABU
Quote
 
 
0 #23 2011-08-04 16:39
Tafiti za kisayansi zinafanywa na wanasayansi. Na kwa utafiti kama huu unaohusu masuala ya tiba ni lazima umpime mgonjwa alikuwa na ugonjwa gani (viral, bacterial, metabolic n.k). Then unampa dawa na baada ya muda unampima tena kuona kama dawa imefanikiwa kuua hao wadudu au ugonjwa huo. Na utafiti kama huo unafanyika maabara. Sasa tunahitaji kujua, kwanza taaluma za hao watafiti wa synovate na methodology waliyotumia kuhakikisha kwamba hao wagonjwa walikuwa na ugonjwa fulani na wamepona baada ya kutumia hiyo dawa ili tusiendelee kupotosha watu wengi zaidi.
Quote
 
 
0 #22 2011-08-04 15:39
babu alitaka miundombinu ijengwe wilayani kwake coz serikali ilikuwa imesahau
kumbukeni ideology ya maji kuyeyusha risasi kwenye majimaji war na kinjekitile ngwale
Quote
 
 
0 #21 2011-08-04 15:04
hatudanganyiki! hatuachi hoja ya mafisadi ng'o! sinovate mnalipwa na CCM kwenye uchaguzi mlitumika sana! mnatia aibu. utafiti huu hata kalimanzira anaweza, no science!
Quote
 
 
+1 #20 2011-08-04 15:03
Unajua hakuna kitu kigumu kama imani na cku zote unachoamini ndicho kitakachokutoke a binafsi cjawah kwenda huko ila naamini Babu anaponya na mnaowabeza Synovate think twice wanafanya kazi kuisaidia na kuielimisha jamii n c vinginevyo babu anaponya kwa imani yako na dawa zake ni mitishamba.Jaribu kuchunguza hao raia mwema wamefanya uchunguzi wapi na wapi?Tujenge nchi co bla bla na utoto tunapocomment tufikirie mara mbili ni kwa ajili ya jamii ya Kitanzania
Quote
 
 
0 #19 2011-08-04 15:01
Quoting Sam:
Non scientific research!
Such kind of researches have no benefit to the public!

MAABARA YA NINI KAMA MTU ALIKUWA ANAUMWA NA SASA AMEPONA, WHAT KIND OF SCIENTIFIC TEST ARE YOU AFTER?? MBONA WATU WANATUMIA MADAWA YA KISAYANSI NA YET WANAKUFA. ACHA FIKRA MGANDO. BABU YUKO JUU NA KIKOMBE CHAKE
Quote
 
 
+1 #18 2011-08-04 14:59
Hii taasisi ya Synovate imejaa ubabaishaji. Yaani unamuuliza mgonjwa kuwa baada ya kunywa kikombe umepona au la. Nafikiri njia bora ni kuwapima maradhi waliyokuwa nayo ndiyo kigezo cha kujua kama mtu amepona au la. Binafsi ninawajua watu waliotumia dawa hiyo na hali zao kiafya si nzuri
Quote
 
 
+3 #17 2011-08-04 14:14
Ahsanteni sana kwa wale wasioamini kutambua na kuelewa kuwa BABU anatibu.Hii ya kuamini ni kwa wale waliofika na kunywa kikombe huku wakiamini kuwa wanaumwa na watapona.Inmasikitisha kuona mtu ambaye hajawahi kwenda kwa babu kusimama juu ya jukwaa la mitaani akipinga uponyaji wababu.SWALI:- KUNA MTU AENDAYE PENYE UTATUZI WA MATATIZO (mfano;hospital i,mahakamani,po lisi au sokoni) PASIPOKUWA NA TATIZOLA KUMFANYA AENDE HAPO? kama mtu anaenda maeneo hayo bila sababu za msingi basi [NENO BAYA].Wagonjwa nendeni mkapone kwa jina la Mungu
Quote
 
 
+3 #16 2011-08-04 13:33
Ni sawa na dawa za hosp,wewe unaweza kupona,ila mwingine asipone.Akili kumkichwa hapo
Quote
 
 
-2 #15 2011-08-04 13:24
Non scientific research!
Such kind of researches have no benefit to the public!
Quote
 
 
+1 #14 2011-08-04 13:06
nyie watu mnaomlaumu babau kwanza namba mooja nainyi ni wachawi.it had to do with faith...na kumbuka babau mweneywe alisema wagonjwa waliozidiwa yaani walioko kwenye criticala condition wasiende...kwani alaiwalazimisha waende>>>>wewe fikiria mgonjwa anatolewa ICU huko kigoma ...atafika saa ngapi arusha na unakuta kwamba hajasafiri hata na mhudumu wa afya kwa ajili ya kumtake care/
wenh=gi waliokufa ni wale ambao walikuwa wamezidiwa sana.mbili wale ambao ni wachawi...usisahau pale babu alikuwa ana tumia nguvu za mungu...kama wewe ni mchawi na unaroga na kuua watu sasa ni kwanini wewe unatakla kupona kama kuua si kitu kibaya ni kwanini wewe mchawi hutaki kufa?/ yale yalikuwa mambo ya kiimani zaidi na tusihukumu sana maana atutahukumiwa tusipoangalia...hakuna mtu ana uhakika ZAIDI KWAMBA NUI NINI HASWA KILIFANYIKA ILA MUNGU SI MWANADAMU MANA YEYE ANAJUA YOTE.
Quote
 
 
+1 #13 2011-08-04 11:55
hhh
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner