MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Dk Hosea aula AU, sasa kuzuia rushwa Afrika
BOOKMARK THIS PAGE
Dk Hosea aula AU, sasa kuzuia rushwa Afrika  Send to a friend
Thursday, 02 February 2012 21:30

Leon Bahati
UMOJA wa Afrika (AU) umemteua Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk Edward Hosea kuongoza Secretarieti ya Bodi ya Kuzuia Rushwa Barani Afrika.AU pia imeteua makao makuu ya Sekreterieti hiyo kuwa mjini Arusha, ambapo shughuli zake zote zitaratibiwa.

Akizungumzia kuhusu uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema ulifanywa na AU katika mkutano wake uliomalizika hivi karibuni mjini Addis Abba, Ethiopia.

Alipoulizwa mambo yaliyoifanya Dk Hossea  na Tanzania kupata heshima hiyo wakati ambapo Taifa limekuwa likikabiliwa na misuguano ya rushwa, Membe alisema:

“Uhuru huo wa kuruhusu mijadala ya rushwa nchini ndiyo yanayoijengea heshima Tanzania. Hii inaonyesha uwazi wa mapambano dhidi ya rushwa.”Alisema kwamba rushwa ipo sehemu nyingi duniani lakini ni nchi chache zinazotoa uhuru wa wa kuzungumza mambo hayo hadharani kama ilivyo Tanzania.

“Vyombo vya habari vimekuwa huru... Kuwepo kwa mijadala, misuguano, kunatoa fursa ya kuweka sera na mipango ya kukabiliana na rushwa,” alisema Membe.

Katika hatua nyingine Membe alisema kwamba AU imeshindwa kumchagua Katibu Mkuu wa Umoja huo baada ya aliyekuwa anatetea nafasi hiyo, Jean Ping wa Gabon kukataliwa kwa kura.

Membe alisema uchaguzi huo sasa utafanyika Julai mwaka huu mjini Lilongwe, Malawi na kuna uwezekano mkubwa wa katibu mpya kutoka katika nchi za Kusini mwa Afrika.Wakati huo huo, Membe alisema kwamba AU imekasirishwa na kitendo cha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuwaandama viongozi wa Afrika peke yao, huku wakiwaaacha wa mabara mengine.Kutokana na hali hiyo wametaka ICC ifanyiwe marekebisho ili iweze kuendesha shughuli zake kwa haki duniani.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
+2 #6 2012-02-03 15:21
katika watu wote wamemwona Dr. Hosea?? kweli AU imekwisha..........:((
Quote
 
 
+5 #5 2012-02-03 12:44
AU bure kabisa,mtakumbu kwa mlivyokaa kimya mgogoro wa Libya au mlikuwa mnamuonea wivu Gadafi alivyokuwa karibu na watu wake kwenye suala la huduma?
Quote
 
 
+1 #4 2012-02-03 12:37
Huu uteuzi ni wa kisiasa mno kuliko utendaji,Hosea huyu hana sifa za kuongoza mapambano ya Rushwa ktk bara hili.

Waafrika walitakiwa kuangalia katika nafasi yake ya sasa amefanikiwa kiasi gani katika kutokomeza rushwa Tanzania.
Nchi hii hata kupata kikombe cha maji inabidi utoe rushwa iweje leo kiongozi wa kitengo hicho anapata promotion?
Quote
 
 
+1 #3 2012-02-03 12:11
mimi sidhani kama Hosea anafanya kazi yake vyema hapa Tanzania. Mbona hawachukulii hatua wale wote walioshikwa na rushwa hapa kwetu?Mfano hiyo ya rada mpaka mataifa ya Ulaya yameingilia kati na yakaseme kuwa kuna watu waliiba pesa katika ununuzi wa rada muwachukulie hatua.Lakini tumeona kimya.
Quote
 
 
+1 #2 2012-02-03 11:01
Kweli AFRICA NI SIKIO LA KUFA!!!
Hainiingii akilini kusoma na kusikia kuwa kati ya watu makini waliopo kwenye orodha ya kupambana na rushwa na Dr Hosea yumo,au Tanzania nasi tumo.
Kama hiyo haitoshi,Eti Tanzania tunapiga kelele,Je mbona PCCB haina chochote ilichowahi kufanya?
Lakini hii,inaweza kuwa ni janja ya Serikali ya CCM,katika kujisafisha kwa wananchi kuwa japo sisi tuna rushwa lakini bado tunayo nafuu kuliko wenzetu.
Binafsi nasema,Dr Hosea HAFAI HATA KUWA MKUU WA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA WA NYUMBA 10.Kwanza ni mla rushwa mkubwa yeye.Kama anabisha asema nimchanechane hadharani kweupe bila huruma!!!
Quote
 
 
+1 #1 2012-02-03 10:22
AU,hvi Mliwaza nini?HOSEA rushwa ya Tanzania imemshnda,sembu se hyo ya Afrika?mngeiangalia tanzania kwenye Afrika mash ni ya ngapi?
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner