MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Uchunguzi kashfa ya Uda wakamilika
BOOKMARK THIS PAGE
Uchunguzi kashfa ya Uda wakamilika  Send to a friend
Thursday, 02 February 2012 21:36

Patricia Kimelemeta  
KAMPUNI ya KPMG iliyopewa jukumu la kuchunguza mchakato wa uuzwaji wa Hisa za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), imekamilisha ripoti yake itakayoikabidhi kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG), wakati wowote kuanzia sasa.  

Kampuni hiyo ilikuwa ikichunguza uuzwaji wa shirika hilo kinyume na taratibu, jambo lililosababisha Waziri Mkuu,Mizengo Pinda kuunda tume ya kuchunguza uuzwaji wake ambapo alizitaka Taasisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pamoja na  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali(CAG), kuchunguza mchakato mzima wa uuzaji wa hisa hizo kwa Kampuni ya Simon Group Agosti mwaka jana.  

Akizungumza na Mwananchi kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Ludovick  Utouh alisema kuwa, kwa sasa ripoti hiyo imewasilishwa Makao Makuu ya Kampuni ya KPMG nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuihakiki na kuangalia ubora wa ukaguzi wenyewe ndipo waikabidhi kwake aweze kuipitia.  

Alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa na utaratibu wa kuhakiki kazi waliyopewa kabla ya kuiwasilisha kwa walengwa, hayua inayosaidia kuangalia ubora wa kazi husika ili ripoti hiyo ili iwe bora zaidi.  “KPMG wamemaliza kazi yao na kuwasilisha Afrika Kusini kwa ajili ya kuihakiki kabla ya kunikabidhi, kutokana na hali hiyo ninaamini kuwa ripoti hiyo ni bora na iko kwenye kiwango kinachokubalika,”alisema Utouh.  

Aliongeza kuwa anatarajia kuipata ripoti hiyo wakati wowote kuanzia sasa ili aweze kuipitia na kuiwasilisha serikalini kwa ajili ya hatua zaidi.  Alisema kwamba ripoti hiyo ilitakiwa kuwasilishwa Januari mwishoni, lakini kinachofanyika sasa ni kuhakiki zaidi ili iwe kwenye kiwango kinachokubalika.   Utouh alisema kuwa KPMG ni miongoni mwa kampuni zinazoanya vizuri kwenye kazi hiyo na kwamba, hakuna mashaka yatakayoweza kujitokeza juu ya utedaji wa kazi zao, bali kinachotakiwa kufanyika ni kusubiri wakati wa kuiwasilisha serikalini.  

Agosti mwaka jana, Serikali ilibaini kuwepo kwa ukiukwaji wa kisheria katika uuzaji wa UDA jambo lililosababisha kuundwa tume ya kuchunguza hatua zilizotumika. Baadhi ya viongozi wanaohusika na uuzaji huo ni pamoja na Mwenyekiti wa UDA, Idd Simba, Meneja Mkuu Victor Milanzi, ambapo kwa pamoja wanadaiwa kuwa waliamua kutafuta mwekezaji binafsi ili aliendeshe shirika hilo kwa faida.

Kabla ya ubinafsishaji huo, UDA ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu, kupitia Hazina, wakiwa na jumla ya hisa 15 milioni ambapo kila hisa moja ilikuwa na thamani ya Sh100.

Kwa mchanganuo, Halmashauri ya Jiji ilikuwa inamiliki asilimia 51 ya hisa hizo, huku Hazina ikimiliki asilimia 49.


Februari 11, Bodi ya Wakurugenzi ya UDA, chini ya Idd Simba, ilikutana na uongozi wa Simon Group ikiongozwa na Kisena na kusaini mkataba, ambao ulithibitisha kwamba UDA ilikuwa imeiuzia Simon hisa milioni 7.8 sawa na asilimia 52.535 ya hisa.

Mkataba huo ungeifanya Simon Group kuwa mwanahisa mkubwa katika umiliki wa UDA kwa vile Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Hazina, wangebaki na hisa milioni 7.7, ambazo ni sawa na asilimia 47.465.

Baada ya mkataba kusainiwa, kipengele cha kwanza kiliitaka Simon Group kulipa asilimia 25 ya fedha za ununuzi wa hisa za UDA (Sh bilioni 1.142) ambazo ni sawa na Sh milioni 285.669, ndani ya siku 14, tangu kusainiwa ili kuufanya mkataba utambulike kisheria, na Simon Group ililipa fedha hizo siku hiyo hiyo.

Kwa vile fedha hizo zililipwa Februari 11, baada ya siku 14, vipengele vya mkataba vilipaswa kuanza kushughulikiwa kisheria na hasa namba 4.5 ambacho kiliielekeza Bodi ya UDA, kuitisha mkutano wa wanahisa ndani ya siku 14 ili kushughulikia mambo makuu matano muhimu.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner