
| Ewura: wahujumu wa mafuta sasa kukiona | Send to a friend |
| Thursday, 02 September 2010 22:20 |
|
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imeingiza nchini mitambo ya kisasa ya kudhibiti uchakachuaji wa aina zote za mafuta katika vituo mbalimbali. Kwa hatua hiyo, Tanzania sasa inakuwa nchi ya pili katika bara la Afrika baada ya Uganda, kuanza kutumia mitambo hiyo. Mitambo hiyo iliyoanza kufanya kazi tangu juzi, inayawekea alama mafuta wakati yanapojazwa kutoka kwenye tangi la lori la kubebea mafuta, kutoka kwenye maghala yanayotumika katika kuyahifadhia. Hatua hiyo baada ya Ewura kutiliani saini na mkandarasi mmoja wa nchini Canada, aliyepewa jukumua la kuweka vinasaba katika mafuta ya petroli ili yaweze kung'amuliwa mara moja pale yanapochanganywa visivyo halali ua yasipolipiwa kodi na kutumiwa kinyume na sheria. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Meneja Ufundi (Petroli) wa Ewura, Gerald Maganga, alisema mamlaka yake kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeanza kuweka kwenye mafuta,alama ya kikemikali isiyoonekani kwa macho. Alisema alama hiyo inawekwa katika mafuta ya petroli, dizeli na yale ya taa. "Tulianza kutumia utaratibu huu mpya jana (juzi) na unazingatia sheria ya Ewura ya Petroli namba 210/2010," alisema Maganga. Alisema alama hiyo haionekani kwa macho ila kwa kutumia ving'amuzi vinavyotumia teknolojia ya X-ray. Maganga aliongeza kuwa alama itakayotumiwa kwenye mafuta ya taa ni ya kipekee wakati alama nyingine inatumiwa katika mafuta yote yanayoruhusiwa kutumika nchini na kulipiwa kodi. "Mpango huu utawezesha utambuzi au ung'amuzi wa uchanganyaji wa mafuta mengine na mafuta ya taa na matumizi ya mafuta yasiyolipiwa kodi,” alisema Maganga na kufafanua kuwa; Alisema vifaa hivyo vipya vinauwezo wa kusoma kama mafuta hayo yamechakachuliwa au la |













