MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Siasa Ndugai: Tutajadili kufuta posho mpya za wabunge
BOOKMARK THIS PAGE
Ndugai: Tutajadili kufuta posho mpya za wabunge  Send to a friend
Tuesday, 17 January 2012 21:29

Waandishi Wetu
NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wanaangalia uwezekano wa kufuta nyongeza mpya ya posho za wabunge ndani ya siku 10 zijazo, lakini akawashambulia watu wanaoshikia bango nyongeza hiyo aliyoifananisha na tone la maji ikilinganishwa na  mamilioni ambayo alidai vigogo wa mihimili mingine ya dola wanalipana.

Kauli hiyo mpya ya Ndugai inakuja kipindi ambacho nyongeza hiyo ya posho imeibua mjadala mzito, ambao hivi karibuni Naibu Spika huyo alilazimika kujibu mapigo ya Waziri Mkuu Mstaafu,  Frederick Sumaye ambaye alionya kuwa posho hizo zinaweza kufanya taasisi nyingine za dola kudai nyongeza.

Juzi, Ndugai akizungumzia posho hizo alisema hazilingani kwa namna yeyote ile na posho wanazopewa viongozi wastaafu serikalini na Idara ya Mahakama.

Alipomjibu Sumaye kuhusu suala hilo la posho, alimshambulia  kiongozi huyo mstaafu akisema hana usafi wa kuzikosoa kwani aliwahi kufanikisha Sheria ya Mafao ya Viongozi Wakuu Wastaafu ili kujiandalia mazingira ya kula maisha mazuri.

“Hili la posho limesemwa sana na sisi tumelisikia kwa sababu ni wasikivu, kumekuwa na kelele nyingi za posho. Kwa kuwa  tunakutana siku 10 kabla ya kuanza kwa Bunge, tutakaa na kulijadili kisha tutasema tumefikia wapi,” alisema Ndugai wakati akizungumza katika Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Alisema Watanzania wanapaswa kutambua kuwa posho wanazolipwa wabunge ni kidogo ikilinganishwa na mihimili mingine ya dola huku akienda mbali na kuwagusa viongozi wa dini kwamba kuna baadhi ya maaskofu na wachungaji wanaopiga kelele  kuhusu posho hizo za wabunge bila kujua wanalipwa shilingi ngapi au zinatofautiana vipi na wachungaji wengine.
“Kuna maaskofu ambao wamekuwa wakipiga kelele juu ya hizi posho, lakini hata na wao ukiwaangalia kuna tofauti kubwa sana kwao na wachungaji katika mapato yao,” alieleza Ndugai:

Alisema wakosoaji wamekuwa wakilalamika tu bila kutoa suluhu au njia ya kutatua hali hiyo ikiwa ni pamoja na kupendekeza kiasi cha posho kinachopaswa kulipwa na kushauri kuwa taifa liunde  kamati maalumu ya kuchambua na kuweka bayana viwango vya  mishahara ya viongozi na posho zao ili kila mwananchi aweze kuvitambua.

“Wananchi wanalalamikia sana posho za wabunge kwa kuwa ndicho kitu kidogo wanachojua ambacho wameambiwa na magazeti, lakini wangejua viwango vya posho wanazolipana watu wa Mahakama na viongozi wetu wastaafu, wangeachana kabisa na hili suala la posho za wabunge,” alisema.

Alisema pia mishahara ya wabunge ni tone tu la mshahara wa ofisa wa kawaida wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisa wa ngazi ya chini wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Ndugai alisema kelele hizo za wananchi zinachangiwa zaidi na hali ngumu ya maisha waliyo nayo kwa sasa... “Kama nyumbani kuna chakula kidogo, ukipika nyama na kuwagawia watoto wako finyango mbili tatu wataanza kugombea, huyu kapewa kikubwa na huyu kapewa kidogo.”

“Wenzetu wa Kenya na Mauritius wana tume ambayo ni huru na ina watu ambao wanaaminika kuwa ni waadilifu, ndiyo wanaangalia mishahara ya viongozi wa juu kama hapa kwetu labda ni kuanzia kwa mkuu wa mkoa mpaka hata Rais. Ukienda kwenye mtandao  unaona kila kitu, hakuna usiri, tupate chombo huru ambacho kitatupangia sisi wote ambao tunapata pesa kutokana na kodi za wananchi... nasema Watanzania wangejua maeneo mengine kukoje wangeachana kabisa na suala la posho za wabunge.”

Alipoulizwa kama angetaka tume hiyo ipunguze posho zilizopo, alisema ingekuwa vizuri kama ingepandisha zile zilizo chini ili angalau kuwe na uwiano... “Lakini kama ikibidi sawa, ila ndiyo yatakuwa yaleyale kuwa huyu ana nyama kubwa zaidi.”

Kuhusu posho zenyewe
Kwa mara ya kwanza Novemba 28 mwaka jana, gazeti hili liliripoti kupanda kwa posho hizo za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 kwa siku walizokuwa wakilipwa awali, mpaka kufikia Sh200,000.

Hata hivyo, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah alikanusha vikali habari hiyo, lakini siku chache baadaye Spika wa Bunge, Anne Makinda alithibitisha kupandishwa kwa posho hizo ambazo wabunge walianza kulipwa katika mkutano ulioisha.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa kila mbunge analipwa zaidi ya Sh7 milioni kila mwezi, ikiwa ni mshahara pamoja na posho nyingine.

Jumuisho hilo ni pamoja na posho ya mafuta Sh2 milioni kwa mwezi ikikadiriwa kuwa atatumia lita 1,000 ambazo makisio ni Sh2,000 kwa lita moja. Nyingine ni posho ya kukaa jimboni Sh800,000 posho ya ubunge Sh1 milioni, kuendesha ofisi Sh700,000, simu Sh500,000 na mshahara ni Sh2.3 milioni.

Wakati wa vikao bungeni, kunaongezeka nyingine za aina tatu ikiwemo ile ya ‘sitting allowance’ ambayo sasa ni Sh200,000 posho ya kujikimu Sh80,000 na usafiri Sh50,000 ambayo hupewa bila kujali kuwa tayari kuna fedha za mafuta ya mwezi mzima.

Habari hii imeandaliwa na Fredy Azzah, Fidelis Butahe, Ibrahim Yamola na Keneth Goliama.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #31 2012-01-19 18:58
Hiv Ndugai si mbunge ! nakazi ya mbunge si kumtetea mwananchi na Rasilimali zake? sasa iweje aone mwingine anazitumia vibaya na yeye aingie kwenyekundi hilo ! tena kwakusema tunamlalamikia yeye kwakuwa hatujawaona wengine ,Hiv ni hakii ! kwanini asituoneshe na kuwakemea badalayake anajiunganisha nao . . . .
Quote
 
 
0 #30 2012-01-19 17:07
Nampongeza naibu spika kwa uelewashaji wake. Mimi ni mjasiliamali Tanzania hii,je katika ufafafanuzi wa mheshimiwa ni wapi WATANZANIA WENZANGU MMEONA ANAONGELEA POSHO ZA WALALA HOI KAMA POLISI WANAOLALA BENKI WAKILINDA HIZO PESA?WALIMU WANAOSHINDA NA WATOTO WAO? jua tu wanaongelewa TRA,TANAPA na vigogop wengine.AHSANTE NAIBU KWA ELIMU YAKO KWETU SISI WASIOELEWA TANZANIA INAENDA WAPI!!!!!!!!!!! !!!!!!!
Quote
 
 
0 #29 2012-01-19 00:59
Nikweli mh.Ndugai anapaswa kuwa makini na kile anachokiongea.Kwamaanahiyo ameingia madarakani ili aweze kugombea hizo posho si kupigania maslahi na maisha ya watanzania kwa ujumla.Awe makini asijisahau kwani yupo bungeni kwaajili ya maslahi ya walio wengi.
Quote
 
 
0 #28 2012-01-18 23:03
yan inaasikitisha kiongozi kama huyu ndugai sijui hata alipataje unaibu spika,,haioneka n hata sababu nya msingi kupandisha posho ya wabunge unaongelea watu wengine,,eti maaskofu mara unahamia mihimili mingine yaan wewe unaongea kama mtu asiye namadaraka unalalamika tuuuu,,,suala la chombo huru ni wewe kuanzisha bungen iweje ss nawe unatwambia sisi wananchi tena? nan aombe hilo lifanyike? jaman sina uhakika na maneno ya ndugai kama ni jazba ama ndo uwezo wake wa kufikiri ni namna hiyo na kwa mtindio huuu kaz ipoo
Quote
 
 
0 #27 2012-01-18 22:42
Quoting mtz:
kuwafananisha wabunge waliochaguliwa na wafanyakaz walioajiriwa kutokana na kisomo chao sii sawa,mh.anapaswa kuelewa hao aliowataji ni wataalam wanaofanyakaz kutokana na elim yao lazima walipwe gali,wana siasa hawapaswi kulipwa pesa nyingi kwa vile wao wamechaguliwa na wananch tu hamna utaalam wowote kwenye siasa sanasana porojo tu na maneno mata yasiyotekelezek a wawapo kwenye majukwaa ya siasa.ifike mahali hata mawazir wasiteuliwe kutokana na wanasiasa.bora waajiriwe kama wataalam.siasa zibaki kwa wabunge tu.

Aise nd yangu hii ni bonge lapointi,unajua ingekua vizuri kwani uoni mtu anataaluma ya daktari anakua waziri wa ulinzi,wapi nawapi,mtu kapiga shule chuo kikuu ana hadi master anakuja kuongozwa na mtu ambao ata chuo akifahamu kisa mfanya biashara.imefika wakati kweli iwe ivyo
Quote
 
 
0 #26 2012-01-18 20:20
BUNGE LIMEJIONGEZEA POSHO KWA SABABU KUNA MIHIMILI INAYOPATA ZAIDI AU KULIKUWA NA ULAZIMA. WANANCHI WENGINE WAMEONGEZEWA NINI, NDUNGAI ATUELEZE. HAYO MAONI YAKE ILIKUWA AYATOE MAPEMA SIYO BAADA YA WANANCHI KUPIGA KELELE.
Quote
 
 
0 #25 2012-01-18 19:46
Katika Katiba mpya tuweke ukomo wa mtu kuwa Mbunge. Kwani mtu akijua kwamba atakaa kwa muda gani hatatetea maslahi binafsiya kujiongezea posho bali atajali zaidi maslahi ya wale waliompeleka kwenye Bunge.
Kazi ya Bunge ni kutunga Sheria na kusimamia Serikali. Kama Mheshimiwa Naibu Spika Ndugai alikuwa Bungeni walipojadili na kupitisha maslahi watakayolipwa Wastaafu wa ngazi za juu Serikalini na Mahakama angelikataa wakati ule. Yeye aliliunga mkono wakati huo. Basi Bunge likae na kurekebisha Sheria hiyo ambayo leo anaiona ina mapungufu. Hiyo ndiyo kazi ya Bunge.
Quote
 
 
0 #24 2012-01-18 19:18
Mh.Ndungai inabidi ajue kwamba kama Mh.Sumaye hana usafi wa kuzungumza basi asiongee na awaache nyinyi muweke uchafu wenu? Hiyo ni akili ya wapi? It is time they need to understand, that more than 60% of Tanzanians are well educated to understand the facts. He agrees that some leaders are getting too much, does he even know his job as mbunge? He needs to regulate that!!!! As a member of CCM i can say one thing...i will only vote for the candidate who has the right vision for our country and ready to put our country FIRST. YOUR RECORD WILL COUNT!!! ONE THING MOST OF OUR POLITICIANS DON'T KNOW, BUT THE LATE MWALIMU NYERERE KNEW WAS KNOWING THE TIME "KUJUA NYAKATI". I will run for office one day..because i have the vision of where our country should go.
Quote
 
 
0 #23 2012-01-18 17:16
Jamani!! Upendo umepungua baina ya watu wa aina mbalimbali. Binadamu wote ni sawa, hivyo wote wanahitaji kula, kuvaa, na kulala mahali pazuri. Watumishi wa hali ya chini kama walimu, hawana posho hata kidogo, na mishahara yao ni midogo sana. Je, hawa hawahitaji posho? Wabunge wetu wanang'ang'ania posho maana ni pesa ya ziada, wanaweza kufanyia kitu.Ila naomba kama ni binadamu wafikirie mishahara ya watu wa hali ya chini, na wananchi wanoteseka!!
Kwa sasa imekuwa dili kuingia katika siasa, kwa sababu ya maslahi. Wataalam wengi wanakimbilia huko kwa sababu hiyo.Wabunge muwe na utu, mtumia kauli nzuri na busara!!!
Quote
 
 
0 #22 2012-01-18 15:07
Kwa kuwa ninyi wabunge mmekaa mkatulia wakati hao wengine unaowasema wanajiongezea. Ndiyo maana sisi hatuwezi kukaa mjiongezee. Sisi tuliwatuma bungeni ili mpigee kelele wanapojiongezea , ni kazi ya wabunge kupigia kelele hizo posho unazoziita za mihimili mingine. kwa kuwa hamfanyi hivyo wanachi wanafanya sehemu yao ya kuhakikisha ninyi wawakilishi wao hamjiongezei. labda hilo litasaidia na ninyi kuamka.
Quote
 
 
0 #21 2012-01-18 14:00
hapa mh. Ndugai hana pointi kabisa. Kwanza hakuna taasisi yeyote ambayoofisa wake wa juu (mkurugenzi mkuu) wake anapata hata nusu ya malipo ya mbunge kwa mwezi ya ths 7 milioni kama tulivyoambiwa ndani ya hii makala. Sio TRA, wala TANAPA, wala majaji, wanaopta malipo makubwa hivyo. Tumeona maisha ya wabunge, magari, majumba yao, shule wanazokwenda watato wao, matibabu wanayopta wanapougua nk, sio ya sawa na hao watumishi anaosema.
mbona mheshimiwa Ndugai hazungumzii mamlaka ya hifadhi ngorongoro ambapo ni taasisi yenye mishahar ya juu kuliko zote alizotaja ambapo yeye ameshiriki kupitisha hiyo mishahara ya ngorongoro kwa sababu yeye ni mjumbe wa bodi kwa zaidi ya miaka 6.

Pia hapaswi kuzungumzia suala la kuwepo na chombo cha kuthibiti na kupanga mishahara na marupupu mbali mbali, eti tu kwa sababu posho wa wabunge imepigwa. Bunge ni chombo cha kutunga sheria, kwa nini sikuzote hkuleta hoja hiyo ili sheria hiyo itayarishwa na bunge kupitisha.

Ukweli ni bahati mbaya sana kwamba nchi yetu haina hata kiongozi mmoja mwenye uchungu na matitizo waliyo nayo wananchi wake na pia hakuna nia thabiti ya [NENO BAYA]liza matatizo hayo.
Quote
 
 
0 #20 2012-01-18 13:31
Huyo Ndugai nadhani ni mmoja kati ya watu waliojipenyeza mpaka nafasi za juu lakini hana sifa ya kuwa hapo alipo. Maana mtu mwenye akili timamu na anayejua majukumu yake hawezi kupigania kuongeza posho kwa kutoa sababu za eti za mihimili mingine ziko juu. Yeye kama msimamizi wa serikali alipaswa kuanzisha mkakati wa kuzipunguza posho hizo kama anathibitisha kuwa ni haramu ukilinganisha na uwezo wa uchumi wa taifa. NAMSHANGAA ANAVYOSHITAKI SERIKALI KWA WALIOMTUMI KUISIMAMIA BADALA YA KUELEZA HATUA ALIZOCHUKUA KUKOMESHA POSHO ZISIZOSTAHILI. Shame on him.
Quote
 
 
0 #19 2012-01-18 12:45
Waache walipuane wenyewe kwa wenyewe. Ndugai kwa heshima na taadhima tunaomba ututajie posho na mishahara ya hao watu wa mahakama, viongozi wa dini na hao watu wa taasisi nyingine zinazolipwa mafao kwa kutumia kodi na michango ya wananchi. Tukithibitisha kuwa wanapata kuliko wanavyostahili, tutawashikia bango kama tulivyowashikia ninyi.
hapa ni kukesha tu hadi kieleweke.
Aluta Continua.
Quote
 
 
0 #18 2012-01-18 12:44
sio swala la kuangalia wapunguze ili tuteseke wote kwani hata bei za umeme wameshapandisha
Quote
 
 
0 #17 2012-01-18 12:41
Hili suala la posho ni kero kubwa kwa sababu wabunge, serikali na hata mahakama wamekosa uadilifu na uwajibikaji. Tanzania ni nchi tajiri sana na kama kila mmoja wao angetekeleza majukumu yake kwa kujitoa kwa moyo wote na akili, elimu n.k. kwa manufaa ya nchi tungekuwa mbali sana. Hata hiyo posho ingekuwa kidogo lakini kwa sababu wote wameifikisha hii nchi hapa tulipo na kila mara wanasema nchi ni maskini sana hawastahili kabisa hata hii posho wanayopata.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner