MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Siasa Mtikila kutinga kortini posho za wabunge
BOOKMARK THIS PAGE
Mtikila kutinga kortini posho za wabunge  Send to a friend
Thursday, 02 February 2012 21:32

Hussein Issa,
KITENDO cha wabunge kujiongezea posho kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 bila idhini ya Rais, kimemkera mwenyekiti wa Chama Cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila ambaye sasa amesema anajiandaa kwenda mahakamani kufungua kesi ya kughushi dhidi ya viongozi wa taasisi hiyo ya kutunga sheria.

Mtikila aliliambia gazeti hili jana kuwa kama kweli Rais Kikwete hajasaini posho hizo, basi bunge limeghushi na kuliibia taifa na kitendo hicho hakiwezi kuvumilika.

Alisema tayari ameanza maandalizi ya kesi hiyo kwa kuwatafuta wanasheria wa ndani na nje ya nchi watakaosimamia mahakamani hadi haki itakapotendeka.

Alisema mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo ni Spika wa Bunge Anne Makinda, wa pili ni naibu wake Job Ndugai na baadaye wabunge wote wanaosaini nyongeza hiyo ya posho isiyokuwa na baraka za rais.

"Huku ni kughushi na kuhujumu uchumi wa nchi, Bunge kujiongezea posho bila idhini ya rais! ni wizi wa kawaida kabisa ambao ni kosa la jinai. Niko mbioni kukamilisha taratibu na hakika ninaenda mahakamani," alisena Mtikila.
Kwa mujibu wa Mtikila, mbali na Bunge kesi hiyo pia itamhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Yeye atahusika kwa sababu ameliona hilo na ameendelea kukaa kimya. Huu ni uzembe na sheria zinasema kutenda au kutotenda kunakoleta madhara ni kosa."

Mtikila alisema anasikitika kuona viongozi waliopewa fursa ya kuwatumikia wananchi, wanatumia fursa hiyo kuwajumu na hii haivumiliki.

“Nitaenda mahakamani kwa sababu hili suala sio la mchezo kabisa linaumiza wananchi,” alisema.
Hata hivyo Mtikila hakusema lini atafungua kesi hiyo zaidi ya kusisitiza kuwa bado anaendelea na maandalizi ya kutafuta wanasheria.

Mtikila alieleza kuwa matatizo yanayolikabili taifa kama hili la wabunge kujiongezea posho kinyemela, linatokana na matatizo ya katiba ambayo watanzania wanapaswa kujipanga kuyaondoa katika mchakato huu wa katiba mpya.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
+1 #8 2012-02-03 14:55
Pambana usilegeze kamba nasi tunakuombea.
Quote
 
 
0 #7 2012-02-03 14:53
Rev.fanya mchakato mapema wa kukutana na wajuzi wenzio ili mkomeshe hali hiyo kwani wanachukua maamuz bila kumjulisha hata mkubwa wa nchi.pambana
Quote
 
 
+1 #6 2012-02-03 13:49
SAwa kabisa kamanda mtikila.tuko pamoja
Quote
 
 
+2 #5 2012-02-03 13:10
Mtikila hana wa kumuunga mkono lakini ni mpiganaji japokuwa naye ana matatizo yake. Mgombea binafsi, vibali vya mkutano kwa wanasiasa alipigania huyu
Quote
 
 
+2 #4 2012-02-03 12:40
Rev. hii taasisi inaonekana kughushi ni jambo la kawaida,mkutano uliopita nilisikia wabunge wakilalamika kuwa saini zao zimeghushiwa kwenye posho lkn hakuna hatua tunaisikia kwa mbwembwe kama ilivyo kwa wezi wa kuku
Quote
 
 
+2 #3 2012-02-03 11:45
Babu mtikila wewe mpigania haki tangu ulipopambana na mgombea binafsi.Big up
Quote
 
 
+4 #2 2012-02-03 08:38
Na mkurugenzi wa mashtaka na mkurugenzi wa takukuru nao wawepo kwa kukaa kimya bila kufungua mashtaka, wakishuhudia makosa yanafanyika, maana yake ni kuyabariki
Quote
 
 
+3 #1 2012-02-03 08:09
Big up Mchunngaji. Lakini usimsahau Mizengo katika listi yako......
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner