MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Siasa Waziri atangaza ukata serikalini
BOOKMARK THIS PAGE
Waziri atangaza ukata serikalini  Send to a friend
Thursday, 02 February 2012 21:44

Habel Chidawali, Dodoma
na Boniface Meena, Dar
SERIKALI imekiri kuwa hali yake kifedha ni mbaya, ndiyo maana halmashauri nchini hazina fedha za kuendesha mambo mbalimbali ya kiutendaji.Desemba 6 mwaka jana gazeti hili liliripoti kwamba Serikali inakabiliwa na ukata uliosababisha wizara, idara na taasisi za Serikali zikiwamo baadhi ya vyuo vyake vikuu, kushindwa kufanya baadhi ya kazi zake, lakini Serikali ilikanusha.

Jana, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Singida Magharibi, Mohammed Missanga alikiri ukata huo na kueleza kuwa ni tatizo kubwa.

Missanga alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu ukata uliozikumba halmashauri nchini kwa kukosa fedha kutoka Serikali Kuu, kitendo ambacho kimesababisha zishindwe kufanya mambo mbalimbali ya kiutendaji ikiwamo kuendesha vikao vyake na kusimamia maendeleo ya miradi.

Akijibu swali hilo, Mkuchika alisema  halmashauri zina tatizo kubwa la fedha ambalo linasababisha baadhi ya mambo ikiwemo kufanyika kwa vikao vya kiutendaji kusimama. Aliongeza 'Kiwango cha fedha ni kidogo na hili liko mikononi mwa Waziri Mkuu."

Alisema tatizo hilo ni kubwa mpaka Chama cha Serikali za Mitaa (ALAT) kimeomba kukutana na uongozi wa juu wa Serikali, ili kuzungumzia tatizo hilo.

Mkuchika alisema katika halmashauri zote nchini hivi sasa kuna matatizo makubwa yanayotokana na ukata wa fedha ambazo kwa muda mrefu hazijapelekwa huko, huku akikiri pia hata fedha za mwaka jana hazijapatikana. Katika kuthibitisha tatizo hilo, Waziri huyo pia alishindwa kueleza lini fedha hizo zitapatikana na kupelekwa kwenye halmashauri.

“Hata za mwaka jana hatujapeleka huko ndio maana wanalalamika, hata ALAT wameomba kukutana na uongozi wa juu serikalini kuzungumzia jambo hilo, lakini, kwa ujumla hali ni mbaya,’’alisema Mkuchika.

Ukata huo ulisababisha kuchelewa kwa ruzuku ya vyama vya siasa vyenye wabunge na madiwani, hali iliyoathiri uendeshaji wa shughuli za ndani za vyama hivyo kikiwamo chama tawala, CCM.
 
Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC), Augustino Mrema alisema ukata huo umesababisha miradi mingi kukwama kutokana na bajeti iliyopitishwa kutotekelezeka.

Alisema ni kweli Serikali inayumba kwa kuwa hali ya fedha ni mbaya. "Alichosema  Mkuchika ni sahihi na nampongeza kwa kukiri kuwa hawana fedha kwa kuwa mambo hayaendi kabisa huko kwenye halmashauri."

Mrema aliongeza, "Kwa mfano kule Himo waliniambia  wangenipa Sh150m kwa ajili ya mradi wa maji, lakini hadi hivi sasa wametoa Sh50 milioni ambazo haziwezi kufanikisha mradi huo."

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #16 2012-02-04 09:05
Hapo sana tu;serikali miyeyusho hii.Wananchi tuna hela kuliko serikali yetu
Quote
 
 
0 #15 2012-02-04 08:37
Quoting Judom:
Hili ni jambo zito sana kwa Serekali kukiri hadharani haina fedha, nionvyo mimi kwa imani zetu tuiombee sana hali ya uchumi wa nchi yetu, Na wenye ujasiri wa siasa wasisite kutoa suluhisho kwa ushahuri na kuwashitaki wanaosababisha hali hii.
Toka kwa mtu wa MUNGU

kaka/dada mimi pia ni mwamini. ila kuna sehem nyingine imanihaichukui nafasi kubwa mkuu. hapa tunahitaji strategies za kuokoa uchumi wa nchi sio maombi. ukipita ubungo na mwenge jioni ya saa11 hadi saa2 kama unaufaham uchumi ndo utaua mwelekeo wa hii nchi.kama tumefikia kiasi cha kuuziwa kiatu(ambacho unaweza kuvaa ukatoka)hatakam a ni kwa siku mbili kwa shilingi 500, na kiatu/kijiko/sahani/nguo/urembo/n.k hicho kimetoka nje ya nchi unategemea serikali inamapato gani ya ndani? je ya nje inaweza hata kuyaota? nchi ingekua object ukaiona hii yakwetu tungeona kua imekonda/inakonda kwa kasi ya ajabu mwisho inakufa.
Quote
 
 
+2 #14 2012-02-03 14:53
SERIKALI ILIWEZAJE KUPANGA BAJETI HALI HAINA PESA, NA KAMA PESA ZILIKUWEPO ZIMEKWENDA WAPI? ZIMETUMIKAJE? WATANZANIA TUNADANGANYWA SANA PASIPO KUJIELEWA..!
Quote
 
 
+3 #13 2012-02-03 14:51
msituchanganye akili,fedha zipo.mmeshindwa kazi achieni ngazi.
Quote
 
 
+3 #12 2012-02-03 14:38
Pesa zipo, mbona wao wanalipana sh 330000 kwa siku. Msitufanye wa[NENO BAYA]
Quote
 
 
+1 #11 2012-02-03 13:45
Halmashauri hazina fedha mbona wahasibu wa halmashauri nchini wanajenga majumba kila mwaka?Pesa wanazitoa wapi
Quote
 
 
+2 #10 2012-02-03 13:44
Rasilimali tunazo nyingi tatizo ni mgmnt..mafisadi wanazikamu,
Quote
 
 
+4 #9 2012-02-03 13:20
mimi naona hapa siri inafichuka.nakumbuka wakati mkulo akiambiwa serikari ina hali mbaya ilikana.serikari inapaswa kuwa na vyanzo mbadara kuiingizia mapato.serikari ilekebishe sheria ili tunufaike kwenya madini.haiileti maana kuona wananchi wanateseka na nchi yetu imebarikiwa
Quote
 
 
+2 #8 2012-02-03 12:43
Hali ni mbaya sana kuanzia serikali kuu. Bajeti zinazopitishwa na Bunge mwaka hadi mwaka hazifuatwi kabisa kuna baadhi ya wizara ambazo mpaka sasa mwezi wa pili zimepokea asilimia 10 tu ya Bajeti yake iliyopitishwa bungeni. Sasa 10% itafanya nini? Kazi haziendi kabisa zimekwama. Hizo Posho za wabunge ambazo hazikuwa ndani ya bajeti zimeongezea serikali kuu ugumu wa kupata fedha kwa Wizara za serikali.
Quote
 
 
+3 #7 2012-02-03 12:01
Da!sasa selikari iko wapi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kama safari za nje,gharama kubwa kwenye sherehe,matamas ha egTANZANIA50!th en Mrema toka hapo wape Wenye uwezo wa kuhoji!
Quote
 
 
+4 #6 2012-02-03 11:26
Pinda ofisi yake iko kikaangoni tena!

Sijui sasa atawaeleza kitu gani hawa halmashauri,maa na the other day alikuwa msitari wa mbele katika kufanikisha kulipwa kwa posho na kutengeneza picha kuwa serikali inao uwezo.

Nchi hii imekuwa ikilipa watu posho nyingi kuliko uwezo wake, serikali hii goigoi isiporekebisha mambo haya ya posho ni kwamba itashindwa kila sekta.
Quote
 
 
+3 #5 2012-02-03 11:11
msisahau mtikisiko wa kiuchumi duniani hautaadhiri nchi maskini kama TZ. Pili inashangaza sana kusikia wanauchumi wa nchi wakiongea kama wakulima na wanasiasa. Uchumi wa nchi hautategemea fedha wala mikopo bali uzalishaji wa ndani wa nchi.kupunguza kadiri iwezekanavyo kununua bidhaa nnje ya nchi.
Quote
 
 
+4 #4 2012-02-03 10:20
Pesa zitatoka wapi wakati zinaishia kwenye matumbo yenu? Hata Jk hana mshauri? Maana yeye kila siku ni kuzurura nje ya nchi kama siyo kuchezea fedha ni nini?
Quote
 
 
+5 #3 2012-02-03 10:16
Sasa Posho wanalipana kwa fedha zipi, kama hazina imefilisika?

Serikali iache longo longo, fedha zipo...

Nchi hii haiwezi kukosa fedha...Tanzania ni tajiri sana!!
Quote
 
 
+4 #2 2012-02-03 09:36
Hivi Tanzania tuna serikali ngapi? Upande mmoja serikali ina hela mpaka wanaogezana posho, upande mwingine serikali haina pesa za maendeleo! Mbona mnatuchanganya? Mara TRA wamekusanya 102% mapato, hizo zimeenda wapi? Hivi viongozi wetu, huwa mnawasiliana kabla ya kutoa kauli? Jamani viongozi msituchanganye. Kama serika;i haina hela, basi wote tuonje hilo, kuanzania bungeni mpaka mashambani.Kila mmjoa walau apate kipande cha keki hata ikiwa ni ndogo
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner