MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Siasa Chadema, ZEC waingia kwenye mzozo Z’bar
BOOKMARK THIS PAGE
Chadema, ZEC waingia kwenye mzozo Z’bar  Send to a friend
Saturday, 04 February 2012 08:56

Mwandishi Wetu, Zanzibar
KUMEIBUKA msigano kati ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)  na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu ya ratiba ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Uzini huku ZEC ikiituhumu Chadema kuanza kampeni kabla ya wakati.

Kufuatia hali hiyo ZEC imeiandikia barua ya karipio Chadema, huku chama hicho kikijibu kuwa tume hiyo inapaswa kuwa makini katika utendaji wake, na kuitaka isifanye kazi isiyokuwa yake.

Katika barua yake kwa Chadema, ZEC imekituhumu chama hicho kuanza kampeni kabla ya muda kupitia mkutano wake uliouita wa ndani Januari 27, mwaka huu ambao ZEC imeuita kuwa haramu, ambapo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alizungumza na wanachama wa chama hicho.

Kupitia barua yake ya Februari mosi mwaka huu yenye kumbukumbu namba TUZ/WKATI/BZO/VOL.1/2011/151, ikiwa na kichwa cha habari kisemacho ‘MKUTANO HARAMU ULIOFANYIKA SHEHIA YA TUNDUNI, TAREHE 27/01/2012,”  ZEC imelaani mkutano huo uliokuwa wa hadhara ikieleza kuwa umefanyika kinyume na kifungu cha 34 cha Kanuni za Uchaguzi za 2010.

“Ofisi ya Uchaguzi Wilaya ya Kati kwa masikitiko makubwa inalaani na kukaripia kitendo cha kufanyika kwa mkutano wa hadhara katika maeneo ya Shehia ya Tunduni…siku ya Ijumaa tarehe 27/01/2012, majira ya saa kumi za jioni katika eneo ambalo si afisi ya chama hicho, na kwa mujibu wa mwenendo wa ucahgzui, mkutano huo umetambulika kuwa ni kampeni,” ilisema sehemu ya barua hiyo, iliyosainiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Uzini, Mussa Ali Juma.

Hata hivyo katika majibu yake kwa ZEC kupitia barua ya Februari 3, mwaka huu Chadema ilieleza kusikitishwa kwake na barua hiyo ya ZEC.Chadema ilisema kuwa ZEC imekwenda kinyume cha maadili ya uchaguzi ambayo yanaelekeza kuwa chama au mgombea akifanya jambo lililo kinyume cha maadili, anapaswa kufunguliwa malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi.

“Baada ya msimamizi wa uchaguzi kupata malalamiko hayo, atamwandikia mlalamikiwa akimfahamisha juu ya tuhuma zinazomkabili na kuambatanisha na tuhuma husika. Mtuhumiwa atatakiwa kujibu tuhuma hizo na kuwasilisha kwa msimamizi . Baada ya msimamizi kupokea utetezi wa mtuhumiwa ataitisha kamati ya maadili ili kusikiliza pande zote mbili;…ndipo hukumu hutolewa,” ilieleza barua hiyo ya Chadema kwa ZEC na kuongeza:
“Barua yako haijaambatana na malalamiko uliyopokea na kukusuma wewe kutoa karipio na wala hukueleza kama mlalamikaji ni wewe au ni nani.”

Chadema ilisema kuwa hatua hiyo ya ZEC ni kujigeuza kuwa mlalamikaji, msikilizaji wa malamaiko na hakimu, bila kuhusisha vikao na kinyume cha taratibu  na kwamba kinaondoa imani ya wadau juu ya ofisi hiyo  juu ya uadilifu wake.

Barua hiyo ya Chadema iliyosainiwa na Hamad Yusuf, Mratibu wa Kampeni, Jimbo la Uzini, ambayo gazeti hili liliiona nakala yake ililalamika: “Barua yako ni karipio kwetu na wewe unafahamu kuwa karipio ni adhabu ambayo hutolewa baada ya pande zote kusikilizwa.

Kwa sababu hukutaka kutupatia muda wa kujieleza juu ya tuhuma ambazo hujatufahamisha, tunataka kuiarifu ofisi yako kuwa hukumu yako ni batili kwa kuwa kikao hicho kilikuwa ni kikao cha ndani cha viongozi na wanachama na tume yako kujulishwa ufanyikaji wake

Wakati huo huo, Chadema kimeituhumu ZEC kufanya mabadiliko ya ratiba yanayokibeba Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo kama hayataangaliwa kwa makini, kimedai yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
+1 #1 2012-02-04 13:08
Nyie vibaraka mbona mtatupeleka pabaya. Achaneni ndiyo mzee na fanyeni kazi inavyostahiki. Tendeni haki.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner