MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Siasa Polisi Tanga wazuia mkutano wa Hamand Rashid
BOOKMARK THIS PAGE
Polisi Tanga wazuia mkutano wa Hamand Rashid  Send to a friend
Saturday, 04 February 2012 08:57

Aziza Masoud
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limezuia mkutano wa mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed kwa kile ilichodai kuwa mbunge huyo hatambuliwi na chama chake.

 Mkutano huo uliokuwa ufanyike leo katika Wilaya ya Handeni eneo la soko la zamani Chanika, ulikuwa  na lengo la kwenda kuwaeleza sababu za kufukuzwa uanachama katika chama cha CUF.

Akizungumza na gazeti hili  kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Constatine Massawe alisema kuwa wameshindwa kutoa kibali cha kufanya mkutano huo kutokana na kupata barua ya kutowatambua wanachama  hao kutoka katika ofisi kuu ya chama cha CUF.

“Hakuna kibali cha mkutano wa wanachama wa CUF kilichotolewa kwa sababu tumepata barua kutoka ofisi ya chama iliyoletwa na mwenyekiti  kwamba wamemvua  uanachama huyo kiongozi anayetaka kufanya mkutano,” alisema Massare. Alisema kutokana na hali hiyo hawataweza kuruhusu kufanyika kwa mkutano kwani tayari kunaonyesha kuwa na tofauti kati ya pande hizo mbili ambazo zinaweza zikasababisha vurugu.

Alisema aliongea na mkuu kituo wa kituo cha polisi Handeni awatafute viongozi hao na aongee nao wakipata suluhu wanaweza wakaendelea na mkutano huo.

Awali Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni, Seth Mwakajinga ambaye yeye alisema si msemaji alieleza   kuwa ameshindwa kutoa kibali kwa sababu ya ugomvi uliopo kwani katibu anasema hatambui uongozi huo unaotaka kufanya mkutano.
“Barua yao ilikuwa na maombi matatu ambapo waliomba mikutano miwili na kikao cha ndani kimoja nimezuia vyote mpaka watakapokaa wenyewe na kuelewana na kupata suluhu juu ya ugomvi wao,” alisema Mwakajinga.
Alisema wameshindwa kuruhusu mkutano huo kwa kuhofia kutokea vurugu na kwamba hataweza kuruhusu mkutano huo mpaka wahusika watakapokaa na kuongea vizuri na kukubaliana.

Hivi karibuni mbunge huyo pamoja na wenzake 13 waliingia katika mgogoro jambo lilosababisha kufukuzwa uanachama katika mkutanao wa Baraza Kuu la CUF uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu visiwani Zanzibar.
Tangu kutokea kwa sakata hilo mbunge huyo amekuwa akizunguka katika maeneo mbalimbali na kuwaeleza wanachama sababu ya kuvuliwa uanachama wake.

Kabla ya kufanyika kwa mkutano huo Hamad alikwenda kuweka pingamizi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitoa amri ya kuzuia mkutano huo lakini uliendelea kufanyika.

Mara baada ya maamuzi hayo, Hamad alifungua kesi mahakama Kuu kupinga maamuzi hayo na kesi hiyo bado inaendelea kusikilizwa.Hata hivyo ofisi ya Bunge ilisema bado inamtambua Hamad kama mbunge kupitia chama chake cha CUF. Mwisho.  


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner