MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Membe: Polisi walikiuka maadili mauaji Arusha
BOOKMARK THIS PAGE
Membe: Polisi walikiuka maadili mauaji Arusha  Send to a friend
Tuesday, 11 January 2011 20:57

Hussein Issa  
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema Jeshi la Polisi lilikiuka maadili ya kazi yao, lilipokuwa likikabiliana na raia waliokuwa wakiandamana kupinga suala la uteuzi wa meya wa Arusha.Waziri Membe aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na vurugu zilizozuka baada ya polisi kukabiliana na wafuasi wa Chadema waliokuwa wanaandamana jijini Arusha wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa kwa risasi za moto.

 “Jeshi la Polisi linatakiwa kufanya kazi kwa mipaka ili kuhakikisha kuwa linadumisha amani nchini,” alisema Membe akielezea kuwa ni maoni yake binafsi kuhusiana na tukio hilo linaloelekea kuliwekea doa Tanzania ambayo inajulikana kuwa ni kisiwa cha amani.
 
Vurugu hizo zilitokana na Chadema kuamua kuandamana kwa amani licha ya kuwepo na amri ya polisi iliyokuwa inawazuia wakishinikiza uchaguzi wa  Meya wa jiji la  Arusha urudiwe kwa sababu kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu zilizomsimika Gaudence Lyimo  wa CCM kwenye madaraka hayo.  Membe alisema kuwa mabalozi wa nchi mbalimbali hapa nchini walimbana wakitaka Serikali iweke wazi suala la mauaji hayo ili dunia ifahamu ukweli badala ya tetesi.  

“( Wamenibana (mabalozi) kweli kweli ili Serikali itoe tamko rasmi… Nimewajibu kwamba ndani ya wiki hii Serikali itatoa tamko kwa kuwa nayo haijafurahia mauaji hayo,” alisema Membe.  Aliongeza kuwa waliokufa katika tukio hilo ni Watanzania hivyo bila kujali itikadi ya chama, msiba huo ni wa kitaifa.  

“Natoa pole kwa wafiwa wote ambao wamepoteza ndugu na rafiki kutokana na tukio lile, pia na wale waliolazwa hospitali, nawatakia kila la kheri wapone na kuendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema Membe.  

Membe alisema kuwa jana alikutana na mabalozi hao kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu tukio hilo la mauaji yaliyofanywa na polisi kwenye maandamano hayo ya wafuasi wa Chadema, Januari 5, mwaka huu.  Habari za ndani ya kikao hicho ambazo gazeti hili lilizipata zilieleza kwamba  mabalozi hao walilituhumu  Jeshi la Polisi wakisema kuwa halikutenda haki kwa sababu waandamanaji hawakuwa na silaha na walikuwa wakiandamana kwa amani.

 Walipendekeza pia kuwa ni vyema jeshi hilo likapatiwa mafunzo ya kukabili maandamano ili kujua ni wakati gani wa kutumia silaha za moto, mabomu ya machozi au vifaa vingine vya kutuliza ghasia.

 Chanzo hicho kilieleza kwamba kauli za mabalozi hao kwa kiasi kikubwa zinaweza kuwa zimechangiwa na msimamo wa CCM na Chadema.  Makatibu wa vyama vyote wamesikika wakikebehi kauli iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsa Vuai Nahodha ya kusema tatizo hilo la Arusha ni la kisiasa hivyo linapaswa kutatuliwa kisiasa kwa vyama vyote viwili kukutana na kumaliza tofauti zao.  

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk  Slaa alisema hawawezi kukaa na CCM kwa kuwa chama hicho na Serikali yake ni katili na ya kihuni.  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akasema hawezi kukutana na Chadema kwa sababu suala la meya wa Arusha liko nje ya uwezo wa vyama hivyo viwili.  

Makmba alisema kwamba uchaguzi wa meya ulisimamiwa na Serikali na kwamba wao CCM kama ilivyo Chadema, walichofanya ni kupeleka jina la mtu wanayeona anafaa.  Makamba alifafanua zaidi kuwa kulingana na taratibu, meya huyo wa CCM alichaguliwa kihalali na kwamba kama kuna aliye na malalamiko anapaswa kufungua kesi mahakamani.

Wakati mabalozi wakitoa maoni yao tayari  maaskofu wa makanisa ya Kikristo mkoani Arusha wameshatangaza kutomtambua meya  huyo wa CCM na kwamba hawatampa ushirikiano.
  Kutokana na mazingira hayo ya kuwepo kwa watu waliopoteza maisha na hata shutuma hizo za viongozi wa dini, aliyechaguliwa Naibu Meya, Michael Kivuyo wa TLP, alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi hiyo.
 
Hata hivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameingilia kati sakata hilo kwa kukutana na  Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema na Nahodha. Vilevile, Pinda anatarajiwa kukutana na viongozi wa Chadema.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 07 April 2011 11:22
 

Comments 

 
0 #9 2011-01-13 10:54
Sorry Pinda, you are putting the cart before the horse! Waste not you energy in putting off the fire. Shouldn't you focus on stopping the fire from breaking out in the first place? It is fait accompli: bullets were fired, blood spillt, lives lost! Usipoteze muda kujutia maji yaliyomwagika! Tafuta njia ya kufuta machozi ya waanga, njia ya kuzuia damu ya bure ya wakulima isimwagike tena!
Quote
 
 
0 #8 2011-01-13 10:12
ni kweli umakini wahitajika
Quote
 
 
+2 #7 2011-01-13 10:10
membe amekuwa msemaji wa polisi au ndio anatoa kauli kwa vyombo vya kimataifa hivyo basi kama polisi walikiuka maadili ni hatua gani serikali inachukua kwa mauaji ya kukiuka maadili dhidi ya jeshi la polisi tunataka kusikia IGP anachukuliwa hatua kali kama ndivyo jeshi lilikiuka maadili basi IGP amekiuka maadili pia
Quote
 
 
0 #6 2011-01-13 10:02
binafsi nampongeza sana waziri wa mambo ya ndani kwa kutoa tamko mapema kuhusiana na mauji ya Arusha yalifanywa na police.pia nampongeza waziri Membe pamoja na Wasila.ila nashangazwa na kauli za Makamba ambazo muda wote anapotoa anajificha nyuma ya vitabu vya dini.mimi nashauri hao police waliyofiatua risasi za moto wafunguliwe kesi ya kuua ili sheria ifuate mkondo,hakuna aliye juu ya sheria.
Quote
 
 
+1 #5 2011-01-13 09:59
Hata hivyo waziri Mkuu hakuwa serious katika hili jambo maana limetokea tar 5 january na hadi sasa hajatoa tamko lolote. Matatizo haya yanasababishwa na CCM hasa Makamba ambaye hadi sasa anang'an'gania kuwa uchaguzi ulienda sawa wakati kuna Mary ambaye ni wa viti maalum TANGA amepiga kura ya kumchagua Meya Arusha je tangia lini Mbunge akamchagua Meya kwenye halmashauri isiyo ya kwake? Makamba ni sawa na debe tupu ambalo haliachi kuvuma Tunaomba rais awaondoe kwenye nafasi zao katibu Mkuu, IGP pamoja na Waziri wa mambo ya ndani kwani hawajui wajibu wao.
Quote
 
 
-1 #4 2011-01-13 09:42
Watanzania naomba tuwe wapole kipindi hiki tunachohitaji mabadiliko.
Quote
 
 
0 #3 2011-01-13 08:57
yeah! tunakushukuru sana mueshimiwa waziri kwakuliona swalaili kwani tunauchungu sana tena sana kwakupoteza ndugu zetu wasiokua naatia, iviawa polisi wameshindwa kuzuia nakukabiliana namajambaz nauovuunao fanyika ndani yainchiyetu wanakuja uwawatu wasio naatia kweli? wanastailizabu kalisana.
Quote
 
 
+1 #2 2011-01-13 08:50
MEMBE WACHA KULETA MAELEZO YA KISIASA YASIYO NA TIJA KATIKA SUALA AMBALO LIMEGHARIMU MAISHA YA WATANZANIA, CHA MSINGI UCHAGUZI URUDIWE, NATILIA SHAKA UWEZO WA MAKAMBA KATIKA KUELEWA NA KUCHAMBUA MAMBO, NI NANI HASA ALIYEMLETA HUYU MTU KWENYE SIASA, ALITAKIWA ALIPOSTAAFU JESHI ANGEENDA KIJIJINI KULIMA AU AWE COMEDIAN. NINA HAKIKA HATA MWANAYE JANUARY ANAONA AIBU KUITWA MTOTO WA MAKAMBA, KWANI MZEE HUYU SIKU ZINAVYOKWENDA BUSARA YAKE INAZIDI KUTEKETEA. CCM AMKA, ONDOA MAKAMBA HARAKA KUKINUSURU CHAMA.
Quote
 
 
+1 #1 2011-01-13 08:39
Maskini IGP Mwema, umegeukwa!!!! Unaonekana mbaya wewe sasa, hao ndo CCM banaaa!!!! Imekula kwako hiyo wameshajitoa ingawa yasemekana walikutuma wao utumie nguvu kuua hao waandamanaji Arusha!!! Wamekutia doa, ulikuwa mtu mzuriiii sana ila ndio imeshafutika kwa kutaka kuwafurahisha chama..
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner