MwanzoContactsEmail
Home Habari Mahakamani Wahamiaji haramu wapewa siku saba kuondoka nchini
BOOKMARK THIS PAGE
Wahamiaji haramu wapewa siku saba kuondoka nchini  Send to a friend
Monday, 23 January 2012 19:52

Tausi All
WAHAMIAJIRI haramu wanane kutoka nchi za Pakistan, Bagladeshi na Afrika Kusini, wameamriwa  kuondoka nchini ndani ya siku saba.

Amri hiyo ilitolewa jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.Wahamiaji hao ambao kuondoka kwao kutasimamiwa na Idara ya Uhamiaji, wametajwa ni Rizwan Fazal, Barbar Hussain na Riaz Nagash.

Wengine ni Talha Khaid, Imran Hossain, Habibur Rahman, Esrat Molla na Hussain Amjad.Wahamiaji hao walikuwa wamehifadhiwa katika  maeneo la Kariakoo kinyume cha sheria.Inadaiwa kuwa kitendo hicho kilifanywa kwa ushirikiano wa   Mohamed Fazal na mkewe Fatma Fazal ambao wamehukumiwa  kifungo cha miezi mitatu jela au kulipa faini ya Sh100,000 baada ya kupatikana na hatia.

Wakati huo huo, mahakama hiyo pia imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela,  Issa Mkorea (26) na Abeid Seleman(26) baada ya kupatikana na hatia ya kula njama, kuingilia njia za mawasiliano za TTCL na kuisababishia hasara ya Sh32.5 milioni.

Akisoma hukumu  jana, Hakimu Mkazi, Liad Chamshama ,alisema katika shtaka la kula njama   washtakiwa  watatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Alisema katika shtaka la kuingilia njia za mawasiliano za TTCL na kuisababishia hasara ya Sh 32.5 milioni, watatumikia kifungo cha miaka mitano jela na kwamba katika shtaka la kujipatia huduma kwa njia ya udanganyifu, pia watatumikia kifungo cha miaka mitano jela.

 Hakimu Chamshama alifafanua kuwa vifungo hivyo vyote vitakwenda sambamba  na kwa hiyo  watatumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa kila mmoja.

 Hukumu hiyo ikwisha tolewa na hakimu mstaafu, Ezron Mwankenja Januari 2009 lakini washtakiwa hao na wenzao Maulid Ntandu, Issa ,  Abeid Seleman,  Jumanne Rashid na Salvius Anjelius walikuwa wameruka dhamana na kutoroka.

 Kwa upande wa Issa na Abeid  walitorokea mkoani Singida  hadi walipokamatwa na Inspekta Ally Kimweri na Koplo Elias Israel.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner