MwanzoContactsEmail
Home Habari Mahakamani Mahakama yaamuru wanafunzi watano Mlimani wakamatwe
BOOKMARK THIS PAGE
Mahakama yaamuru wanafunzi watano Mlimani wakamatwe  Send to a friend
Monday, 23 January 2012 19:53

Tausi Ally
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam, imetoa hati ya kuwakamata wanafunzi  watano kati ya 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanaokabiliwa na kesi ya kukusanya isivyo halali, kwa kushindwa kutoa taarifa kuhusu kutofika mahakamani.Hati hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi  Waliarwande Lema, wakati kesi hiyo ilipofikishwa kwa ajili ya kuwasomewa washtakiwa maelezo ya awali .

Hata hivyo hatua hiyo  ilishindikana baada ya wanafunzi hao Baraka Monasi, Godfrey Deogratius, Conel Rwagai, Wilbad Eanes,  Luciana Ismail na wadhamini wao kushindwa kufika mahakamani .

Hakimu Lema aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 13,mwaka huu.Wakati hati  za kukamatwa kwa wanafunzi hao zikitolewa, wanafunzi Rehema Munuo na Rehema Juma walinusurika kukamatwa baada ya wadhamini wao kutoa taarifa kuwa wapo katika mitihani.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa wa 31, inadaiwa kuwa si mwanafunzi wa chuo hicho na kwamba ni kibaka aliyetumia jina la mwanafunzi Said John wakati jina lake halisi ni Hassan Suleiman.

Pia imeibainika kuwa anakabiliwa na kesi nyingine katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.

Novemba 14, mwaka huu, wanafunzi hao walifikishwa mahakamani ambako ilidai kuwa  kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio wa halali na kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo Mlimani.

Hali kadhalika inadaiwa kuwa wanafunzi hao walikaidi amri ya askari  ya kuwataka watawanyike.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala wiki iliyopita alifafanua kuwa kati ya wanafunzi 51 waliokuwa wamefikishwa mahakamani, 43 kati yao ndio waliofukuzwa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #2 2012-01-24 13:51
Katiba inayotakiwa ni ile ya Watanzania wote katika ujumla wao. Isilenge maslahi ya wchache.
Kama katiba mpya ni kwa maslahi ya Watanzania wote, sidhani kama kuna hoja mbaya zinazotolewa na wapinzani kiasi cha serikali kutaka kuendelea na utaratibu na mawazo ya mfumo wa miaka 50 iliyopita.''WE CAN NOT SOLVE A PROBLEM USING THE SAME LOGIC WITH WHICH IT WAS CREATED'' (Stein)
Quote
 
 
0 #1 2012-01-24 11:57
inasikitisha kuona mkandala anashindwa kutumia elimu yake ya utawala. tatizo ni ushikaji na kujuana kwa serikali. tatueni tatizo si kupulizia uturi kwenye uozo.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner