
| Mkurugenzi halmashauri Moshi kizimbani kwa uhujumu uchumi | Send to a friend |
| Wednesday, 25 January 2012 23:10 |
|
Daniel Mjema, Moshi Vigogo hao waliofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Mariam Lusewa ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Annah Mwahalende na Kaimu Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu, Sadik Mrisho. Kwa kawaida kesi za uhujumu uchumi husikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, isipokuwa, zinaweza kusikilizwa na mahakama ya hakimu mkazi kama Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) atatoa idhini. Katika kesi hiyo, tayari DPP alishatoa idhini hiyo Desemba 16, mwaka jana ili tuhuma zinazowakabili vigogo hao ambazo ni kinyume cha kifungu namba 12(3) sura ya 200 ya sheria ya uhujumu uchumi kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, isikilizwe na mahakama hiyo. Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Susan Peter, alidai mahakamani hapo juzi kuwa, makosa yanayowakabili watumishi hao wa umma, waliyatenda kwa pamoja kati ya Desemba 2006 na Machi mwaka jana. Katika shtaka la kwanza, Susan anayesaidiana na Maghela Ndimbo, alidai kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao kwa uzembe wa makusudi walishindwa kumchukulia hatua za nidhamu Mhudumu wa Afya wa Zahanati ya Lole aliyetajwa kuwa ni Frank Lyimo. Waendesha mashtaka hao walidai, licha ya mtumishi huyo kutokuwapo kituo chake cha kazi kuanzia Aprili,2006 hadi Novemba, 2008, washtakiwa hawakumchukulia hatua za nidhamu. Katika shtaka la pili, ilidaiwa kati ya Desemba, 2008 na Machi, mwaka jana washtakiwa hao walishindwa kutimiza majukumu yao kwa busara na kuisababishia Halmashauri ya Moshi kupata hasara ya Sh2.75 milioni. Washtakiwa wote walikana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana kwa sharti ya kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa Serikali mwenye kitambulisho. Washtakiwa hao walitimiza sharti hilo na kesi hiyo iliahirishwa hadi Februari 28, mwaka huu itakapotajwa tena. |
















Comments
Mwanzo mzuri huwa na mwisho mzuri haya ni mashina lazima tuchambue zaidi mti mzima na matawi yake.Tumwogope mung jamii na wananchi wanamatatizo mengi tuwasaidie. Big up TAKUKURU
huu ni unafiki na hakika hamfanyi kazi zenu kama inavyotakiwa iwe.
Mission na vision ya taasisi yenu imebaki kwenye makaratasi tu.shem upon you PCCB!
Jesus come soon! Tufunge macho na masikio.............Hali ni mbaya kuliko tunavyoona na tunavyosikia. Kila mahali ni drama tupu. Nakubaliana nawe.....ipo siku moja kitafahamika tu!