MwanzoContactsEmail
Home Habari Uchumi na Biashara Kamati ya Bunge kuibana Ewura bei ya umeme
BOOKMARK THIS PAGE
Kamati ya Bunge kuibana Ewura bei ya umeme  Send to a friend
Monday, 16 January 2012 20:56

Patricia Kimelemeta na Hussein Issa  
KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imesema itakutana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), kujadili kupanda kwa gharama za umeme huku ikisema itakata rufaa kwenye Baraza la Ushindani Kibiashara kupinga ongezeko hilo.  

Mwishoni mwa wiki, Ewura ilitangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 40.29, hatua ambayo imekuwa ikipingwa na wananchi wengi.  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, January Makamba alisema ongezeko hilo limewaumiza vichwa wabunge, jambo ambalo lilisababisha kamati kukaa na kuijadili.

 Makamba alisema katika mkutano wake huo na Ewura, kamati hiyo itayapatia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Tanesco pamoja na kukokotoa bei mpya na ile iliyopita ili waweze kujua uhalali wake.  “Bei mpya ya umeme imetuchanganya sana, hii inatokana na kuongeza kwa kiasi kikubwa jambo ambalo wananchi wa kawaida watashindwa kuimudu.

Kutokana na hali hiyo, tutakutana na mamlaka husika ili tuweze kujadili na kuangalia hatua zitakazofuata,” alisema Makamba.  Kikao hicho ambacho kimepangwa kufanyika juma lijalo, kitajadili bei hiyo na endapo itaonekana haikustahili watakata rufaa.

Alisema Serikali ilitoa Sh200 bilioni kwa ajili ya kununua umeme, ambazo ni sawa na asilimia 60 ya umeme, huku Tanesco ikichangia  asilimia 40 akisema kama ingeshindwa kutoa kiasi hicho, gharama za umeme zingekuwa kubwa kuliko zilizotangazwa hivi karibuni.  

Viwango vipya Katika ongezeko hilo la bei ya umeme ambalo limeanza kutumika Januari 15 mwaka huu, wateja wa hali ya chini wanaotumia chini ya uniti 50 kwa mwezi, wataendelea kulipa Sh60 kwa uniti wakati watumiaji wa majumbani wanaotumia zaidi ya uniti 50, bei hiyo imepanda kutoka Sh195 hadi Sh273 kwa uniti.  

Watumiaji wa kawaida wakiwemo wenye biashara ndogondogo, bei imepanda kutoka Sh157 hadi Sh221 kwa uniti wakati watumiaji umeme mkubwa wa kati, bei imepanda kutoka Sh94 hadi Sh132 kwa uniti, wakati watumiaji umeme mkubwa hasa wenye viwanda na migodi, bei imepanda kutoka Sh84 hadi Sh118 kwa uniti.

Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), litauziwa umeme kwa Sh106 kwa uniti kutoka Sh83 ikiwa ni ongezeko la asilimia 28.21.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #20 2012-01-17 19:22
Ukimya na unyonge wetu sisi watanzania ndio vinavyosababish a sisi kuburuzwa na serikali pamoja na taasisi zake. Iwe CCM au chama kingine chochote kitakachoingia madarakani hali ya kuburuzana itabaki hivyo hivyo hadi hapo sisi wananchi tutakapokuwa kuwa na uwezo wa kusema basi sasa INATOSHA.
Quote
 
 
0 #19 2012-01-17 18:22
Mafisadi hawa wamezidi. Imefika sasa wanchi tukatae ugandamizaji huu.
Quote
 
 
0 #18 2012-01-17 17:21
huyu mtoto wa makamba amekuwa hovyo kama baba yake. Kazi ni majungu ndani ya CCM. Kila siku anachafua wanasiasa anawaona tishio kwake, amchafue nyalandu,membe, ridhiwani, salva, premi na wengine wengi ili yeye aonekane kijana shupavu. wana bumbuli tumemchoka 2015 kura hatumpi. Ngeleja mfanyie kitu mbaya ili anyamaze, anayumbisha kweli wizara ya nishati. Sasa utetezi wake ni una maana gani? mbona asingetetea kabla umeme haujapandishwa? hatudangayiki. huyu mtu ni hatari kuliko mtu yeyote ndani ya CCM. January tafuta mbinu nyingine. hii ya kutaka kumfanya ngeleja aonekane hovyo haitakufikisha popote. Zaidi utajijengea maandui lukuki
Quote
 
 
0 #17 2012-01-17 16:57
Yaani hawa jamaa wanatukaba kila kona.
Mafuta ya taa bei juu.Gesi ndo haikamatiki,sol a nazo ndo hivyo,Serikali imeamua kutoa adhabu kwa wananchi wake.
Quote
 
 
0 #16 2012-01-17 16:04
Helooo,Nilikuwa nataka uwakumbushe Watanzania wooote Deni letu la Nje,cuz kwakipindi kirefu, kamasiyo tangu kikwete aingie madarakani No one including Mr Kikwete amethubutu kugusia hicho kitu,na dhani unajua nikwanini.Tupe hizo figure Kwenye Gazeti letu nadhani Hao Wabunge wanaotaka kujiongezea mishahara labda wataogopa kidogo.Pia itawapa watu motisha zaidi na mwangaza wapi inchi yetu inaelekea.Please tupia hizo figure online sababu wengiwetu hatupo bongo-Thankssss.Dont post this as comment.
Quote
 
 
0 #15 2012-01-17 15:47
JANUARY NI WA PWANI HAWEZI FANYA KITU CHOCHOTE KUHUSU BEI ZA EWURA KWANI HIZO NI GAME ZINACHEZWA NA CCM MAKAMBA NI BONGE LA MSANII. HII NCHI ITAKUJA NYOOKA TU PALE RAIS KUTOKA KASKAZINI ATAKAPO SHIKA HII NCHI HAWA WAKWERE HAMNA KITU WE MCHEKI JK KAZI KUCHEKAA TU HUKU ANAWABEBESHA WATZ MZIGO WA DOWANS,RICHMOND .EPA MI NWAAMBIA WATZ NI MUDA MUAFAKA WA KUINGIA ROAD KUDAI HAKI LEO HII UMEME HAISHIKIKI HATMA YA MTZ IPO WAPI RAIS KIKWETE NI HASARA KWA WATANZANIA
Quote
 
 
0 #14 2012-01-17 14:55
jaribuni kujadiri jamani suara hili la mafuta lina2umiza vichwa.makamba kaza uzi
Quote
 
 
0 #13 2012-01-17 12:09
makamba mnafiki kamati yake ilifahamu wakati ule serikali imepeleka pendekezo la dharula kupndisha umeme.yeyey mbona wakati ule hakuact mchakato huu umekuwepo ukiendelea akiuona je alifanya nini mpka umeme upande ndo aje na ngojera za unafiki huku akijua rufaa yake ni danganya toto kuwa ghiribu watanzania kuwa alifanyia kazi .
Makamba ajue wantania wa leo si wale wa zamani , yeye na serikali lao moja yeye ni sehemu ya kupandishaw bei ya umeme anachotaka ni kutumia pesa za walipa kodi kufanya vikao kuendelea kuwaghiribu wantanzania wakati rufaa yake ni sawa na kuishitaki dowans
Quote
 
 
0 #12 2012-01-17 11:34
Ufisadi tanesco na wizara ya nishati ni mkubwa kupindukia. gharama za kihuni aina ya richmond na dowans ndiyo zinatumaliza. Kwanza hatujaambiwa nini hatima ya madai ya Dowans! hapa pengine zinatafutwa fedha kuwalipa hao wahuni. Tanesco kuna ufisadi wa wazi na gharama za kifisadi kama za wanasheria waliotuchezesha sheri taifa zima. Wanajidai kimya wanangojea muda muafaka kutukaba koo watutoe kilo ya nyama kwa kulipa mamilioni ya dhuluma. Kama serikali kweli inapinga kulipwa dowans basi wapeleke muswada bungeni kuzuia kulipwa hao wahuni. Mwalimu alipeleka muswada kuzuia Chief Marealle asilipwe fidia kuvuliwa uchifu. Sasa hii serikali ya CCM ifanye hivyo kama kweli wana nia ya kuwalinda wananchi na umafia wa ndani na kimataifa. Sio kuwalundikia wananchi madeni yanayotokana na ufisadi
Quote
 
 
0 #11 2012-01-17 11:22
Sababu za kupanda kwa bei ya umeme linachangiwa sana na shirika la TANESCO kufanya kazi kwa uzoefu.asilimia sitini 60% zinazo changiwa na serikali ni lengo kubwa la kuwasaidia wanainchi na si kusaidia TANESCO.Kwanini bei hizi hazi kupanda kipindi cha uhaba mkubwa wa umeme.kwanini leo.
Naomba serikali kupitia wabunge iwe na msimamo dhabiti ili kumwokoa mwananchi zaidi ambaye ndiye serikali kwa ujumla.
Ni bora likaongezwa shirika jingine zaid ya TANESCO ilikufanya ushindani zaidi ukwele ni kwamba TANESCO ni shirika mfu.
Quote
 
 
0 #10 2012-01-17 11:17
Viongozi wetu tumewazoea, wakisikia kitu kwenye vyombo vya habari ndiyo wanajifanya wazalendo kutaka kuionyesha wanauzalendo wa kuwatetea wanachi wakati kwenye mchakato wanakuwa kimya. Mfano, isue ya kuongezeka kwa bei ya kivuko Kigamboni!!!, Mh. Ndungai...
Quote
 
 
0 #9 2012-01-17 10:38
"wakati watumiaji umeme mkubwa hasa wenye viwanda na migodi, bei imepanda kutoka Sh84 hadi Sh118 kwa uniti..".
Umeme ni mtaji wa wakubwa, kama mafuta taa, dizeli na petroli. Nataka mtu mwenye akili timamu anieleze kwa nini Ewura inawapa wenye migodi ruzuku na kuwakamua wananchi. Inaeleweka gharama za uzalishaji kiwandani zikiongezeka, bidhaa kwa mlaji zinapanda automatically. Gharama za migodi zinamaffect vipi mlaji? Hawa ndiyo waliotakiwa kubeba mzigo wote wa ongezeko la bei kwa sababu ni wanyonyaji wakubwa. Wanatuharibia mazingira na kuilipa serikali kiduchu. Sasa walalahoi wanachangia gharama za kuendesha migodi ambayo haina faida kwao. Serikali ya CCM kweli ni KIZIWI!
Quote
 
 
0 #8 2012-01-17 10:36
nimekuwa nikichangia sana maoni kuhusu umeme,hiini kwa sababu ni muhimili wa maendeleo ya nchi na dunia kwa jumla,jambo la kufanya kwa tanesco ni kuwa wabunifu na kuacha urasimu uliopo ndani ya shirika hili muhimu,kwanza kabisa wananchi wote wapatiwe umeme, hii nina maana kwamba maeneo yote yasiyo na huduma hiyo yapatiwe umeme na si kungoja idadi ya watu iwe kubwa ndiyo wafikirie kupeleka umeme sehemu hiyo,tena kwa kubembeleza!hal i hii inakwamisha maendeleo na shirika kukosa mapato,hii haiingii akilini kusikia sehemu nyingine hapa Dar es salaam hazina umeme hii ni aibu kubwa kwa shirika na nchi kwa ujumla wake,watu wanashindwa kuhamia sehemu wanazojenga kwa sababu ya urasimu ulivyo tanesco,hapo tayari mapato ya shirika yanapungua,na wao kuanza kuongeza bili bila ya kujiuliza ni nini kinapunguza mapato yao,hii tansco lazima wakae na kutafakari kwa makini,wakitaka kuboresha mapato yao wazingatie kupeleka huduma hii pale watu wanapo pimiwa maeneo ya makazi na wao wapeleke huduma yao bila kungoja idadi ya watu na ndiyo wapeleke hiyo huduma tena siyo kwa hiari yao mpaka uwabembeleze!kw a utaratibu huu shirika halitakuja kufanikiwa hata siku moja zaidi ya kupandishia garama wateja ambao ni wachache,hii ni aibu kwa shirika kongwe nchini!
Quote
 
 
0 #7 2012-01-17 10:10
HII SEREKALI HAIWADHAMINI WANANCHI HATA KIDOGO.HAPA NAULIZA TANZANIA KWELI INA RAIS MTETEZI WA WANANCHIN WAKE.KIKWETE JAMANI MKWETUENI SI LAZIMA AMALIZIE HIKI KIPINDI
Quote
 
 
0 #6 2012-01-17 09:44
Shida kubwa juu ya jambo hili kuwa kamati ya bunge na vyombo vya habari ambao ndio tunawategemea mmenyamaza kimya mpaka wanapandisha umeme kimya kimya ndio mnaanza kukurupuka! Mlipaswa kuufahamisha umma juuu ya mpango huu, kelele za wananchi, mavuguvugu ya maandamano, husaidia sana kupunguza maamuzi kama haya ya kuumiza wananchi!

Tunavyojua sisi mpango wa kuongeza bei ya umeme si katika interest ya kuongeza makusanyo ya shirika, kuna mkono wa wanasiasa walafi na wahujumu uchumi ambao siku zote wamekuwa wakinufaika na TANESCO.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner