MwanzoContactsEmail
Home Habari Uchumi na Biashara Maduka ya dawa baridi kufutwa Mei mwaka huu
BOOKMARK THIS PAGE
Maduka ya dawa baridi kufutwa Mei mwaka huu  Send to a friend
Tuesday, 17 January 2012 21:12

Ibrahim Yamola
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) inakusudia kuyafutia usajili maduka yote ya dawa baridi ili kuyafanya yawe  maduka ya dawa muhimu ifikapo mwezi  Mei mwaka huu katika Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Agnes Kijo alisema badala yake yatakiwa kuwapo maduka yenye hadhi ya juu kidogo ambayo yatajulikana kama maduka ya dawa muhimu.
Alisema wameamua kuyafuta kutokana na kutoa huduma zilizo chini ya kiwango hivyo kushindwa kukidhi mahitaji ya jamii na hata yale ya kitabibu kulingana na kanuni za huduma za dawa.

 “Unakuta mhudumu katika duka la dawa baridi hawezi hata kujieleza mwenyewe na pale unapotaka ushauri kabla ya kununua dawa anashindwa kuutoa” alisema na kuongeza kuwa ni hatari ambayo haipaswi kuendelea kuwapo.

Kijo alisema uanzishwaji wa maduka ya dawa muhimu utatanguliwa na mafunzo kwa watoa huduma yatakayofanyika Aprili mwaka huu kwa kipindi cha siku 35 na watakaofaulu mitihani watapatiwa vyeti vya kuhitimu.Alisema mamlaka imeanza maandalizi ya utekelezaji wa mpango huo na tayari wakaguzi 175 ambao watakuwa wakufunzi ngazi za kata katika Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam wameandaliwa

“Tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa tunayaondoa maduka hayo na ambao hawatapata mafunzo hayo ya TFDA na kutunukiwa vyeti hawataruhusiwa kutoa huduma na watakaokiuka utaratibu watachukuliwa hatua za kisheria” alisema Kijo.

Meneja wa Mpango wa Duka la Dawa Muhimu (DLDM), Elizabeth Shakalaghe alisema mfumo huo ukianza kutumika utaboreshwa ili huduma za dawa ziweze kuwafikia walio wengi wakiwamo wa maeneo ya pembezoni.

Alisema Shakalaghe kuwa mpango huo hadi hivi sasa unatekelezwa katika mikoa 15 ambayo nchini na unatarajiwa kusambazwa nchi nzima lengo likiwa kulinda afya za wananchi na kuhakikisha wanapata huduma bora.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #5 2012-01-19 01:06
Ivi huyu meneja wa TFDA kanda ya mashariki anajua alifanyalo kweli?anavunja yaliyopo kwakua hayana hadhi na wauzaji wake hawana uzoefu wa kutosha kwa kulijua hilo ameanzisha kozi maalum ya siku 35 akiwa na imani kwamba muda huo unatosha kuleta mabadiliko kiutendaji kwa wauzaji,anachez a kweli huyu jamani.hili lina shaka ndani yake si bure.
Quote
 
 
0 #4 2012-01-19 00:37
Ni hatua nzuri ambayo TFDA mmeanza kuifanya,naomba kuweka angalizo hamjaweka wazi kwa mfano mwana taaluma ya afya mfano ngazi ya diploma/certificate wakiwemo wauguzi (nurses,Clinica l officers nk,je watahitajika kwenda kozi hiyo ya siku 35 ili kupewa usajiri wa maduka yao? au walengwa hasa wa hiyo kozi ni kina nani?
Quote
 
 
0 #3 2012-01-18 16:36
Yafungiwe yote, huku mawilayani hadi mahouse girl wanauza maduka ya dawa. Au unakuja jamaa anafanya kazi hospitali ya wilaya, na mke wake ni mama wa nyumbani na hana taaluma yoyote. cha ajabu unakuta mama (mrs) ndio muuza dawa. Wanachezea maisha yetu
Quote
 
 
0 #2 2012-01-18 12:38
TFDA mumefanya uamuzi wa busara.lakini pia mnapaswa kuwa makini ili kuepukana na ukiritimba wa biashara ya mlango wa nyuma.
Quote
 
 
0 #1 2012-01-18 11:32
hawa TFDA kwanini kwanza wasingalie maduka yanaoyo endeshwa na serikali kama yanazingatia utaratibu huo au wanataka kuanza ukiritimba ambao utaanza biashara ya mlango wa nyuma. nakusababisha wananchi kupata shida hasa wa vijijini ambako hata mashariti hayo wanayo weka hayatawezekena huko vijijini.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner