
| TRA yakusanya Sh682 bilioni kwa mwezi | Send to a friend |
| Tuesday, 17 January 2012 21:15 |
|
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh682.5 bilioni Desemba mwaka jana na kuvuka lengo la Sh645 bilioni lililokuwa limewekwa.Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Allan Kiula na kufafanua kwamba kiwango hicho hakijawahi kukusanywa na mamlaka hiyo. Alisema Novemba mwaka jana mamlaka hiyo ilikusanya Sh512 bilioni ambazo nazo zilikuwa hazijawahi kukusanywa na mamlaka hiyo. Katika upande mwingine TRA imetoa wito kwa wafanyabiashara wote waliosajiliwa kununua mashine za kielekroniki za kodi kwa kifupi EFDs kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria. Kwa mujibu wa sheria ya VAT, mfanyabiashara yeyote ambaye amesajiliwa na VAT, lakini hajanunua mashine za EFDs au hatumii adhabu yake ni kutozwa faini isiyopungua Sh3 bilioni au kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja. "Wale ambao wamefikisha kiwango cha kusajiliwa na VAT, yaani wanapata mauzo yanayostahili kutozwa kodi ya Sh40 milioni au zaidi, wajisajili bila kukosa,"alisema Kiula. Alisema hadi Desemba mwaka jana, wafanyabiashara 11,140 wamesajiliwa na VAT, na kutumia mashine za EFDs, kati ya wafanyabiashara 12,060 ambao ni sawa na asilimia 92.3. Alisema TRA imeanzisha mkakati kabambe kwa watu wachache wanafuata sheria ili serikali ipate mapato yake stahili.Kiula alisema moja ya mikakati hiyo ni kuwafikisha wahalifu kwenye vyombo vya sheria ili ichukue mkondo wake. |
















Comments