MwanzoContactsEmail
Home Habari Uchumi na Biashara Sh697 bil kutafuta mafuta, gesi Rukwa
BOOKMARK THIS PAGE
Sh697 bil kutafuta mafuta, gesi Rukwa  Send to a friend
Tuesday, 24 January 2012 20:38

Keneth Goliama
SERIKALI imeingia mkataba wa miaka 11 na kampuni za uchimbaji mafuta na gesi maeneo mbalimbali nchini, mradi wenye zaidi ya thamani ya Sh18 bilioni .Mikataba hiyo ilisiniwa na Shirika la Mandeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni tatu, uchimbaji wake utaanza mwaka huu na kumalizika 2023.

Awali, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema kampuni hizo zimeingia nchini kufanya utafiti wa mafuta na gesi sehemu mbalimbali, ikiwamo bonde la Malagarasi, Kyela na kwenye kina kirefu cha bahari.

Waziri Ngeleja alisema kampuni hizo ni kutoka Brazil, India na Uingereza na kwamba, zimeingia mkataba wa kushirikiana kutafuata mafuta kuhakikisha Tanzania inazalisha mafuta kama nchi zingine za Afrika ifikapo mwaka 2023.

Kampuni hizo ni Petrbras Limited (Petrbrs) kutoka Brazil, Motherland ya India na Heritage Rukwa (Hertage) kutoka Uingereza.Ngeleja alisema wamekubali utafutaji mafuta na gesi bonde la Ziwa Rukwa  na Kyela, kutokana na kupatikana kwa mafuta Ziwa Albert, nchini Uganda. Alisema  

Naye Mkurugenzi wa TPDC, Yona Kilagane, alisema mpaka sasa kampuni zilizoomba leseni ya utafiti wa mafuta na gesi ni 28, kati yake 18 tayari zimepata vibali.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner