ACT yataka Serikali kudhibiti mfumuko bei za vyakula

Muktasari:

  • Akizungumza na waandishi wa habari, katibu wa kamati ya maendeleo ya jamii ya chama hicho, Janeth Rithe amesema chama kinashauri Serikali itenge fedha za kutosha katika bajeti ijayo kwa ajili ya Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula(NFRA).
  • Amesema Serikali iwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji ili Taifa liwe na uhakika wa chakula wakati wote.

Dar es Salaam. Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuchukua hatua za kudhibiti mfumuko wa bei za vyakula nchini ambao unazidi kuongezeka sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari, katibu wa kamati ya maendeleo ya jamii ya chama hicho, Janeth Rithe amesema chama kinashauri Serikali itenge fedha za kutosha katika bajeti ijayo kwa ajili ya Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula(NFRA).

Amesema Serikali iwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji ili Taifa liwe na uhakika wa chakula wakati wote.

"Tumefanya utafiti katika mikoa nane, tumebaini bei za unga na maharage zimepanda sana, kwa mfano unga uliokuwa unauzwa Sh900 sasa ni wastani wa Sh1,600 kwa kilo. Hali ni mbaya sana huko mikoani, watu wanashindwa kumudu bei hizo," amesema.