AG ataka vyama vya siasa kuheshimu tamko la polisi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju

Muktasari:

Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo,  Masaju amesema polisi wana haki ya kuzuia mikutano na maandamano iwapo watabaini kuwa yataibuka mambo yatakayohatarisha amani ya nchi.

Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amevitaka vyama vya siasa kuheshimu tamko la Jeshi la Polisi kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo,  Masaju amesema polisi wana haki ya kuzuia mikutano na maandamano iwapo watabaini kuwa yataibuka mambo yatakayohatarisha amani ya nchi.

Huku akinukuu Katiba ya nchi, sheria ya vyama vya siasa, Masaju amesema hakuna suluhisho zaidi ya kusitisha maandamano kwa kuwa hakuna anayeweza kuishauri polisi kuwa katika maandamano na mikutano hiyo amani itakuwapo.

Amevishauri vyama hivyo kufanya mazungumzo katika vikao vya Baraza la vyama vya siasa.

Pia amesema viongozi wa dini wanaweza kushauri juu ya kuheshimiwa kwa mamlaka na si vinginevyo.