ATCL yazidi kujipanga, yatangaza ajira mpya 28

Muktasari:

ATCL imetangaza nafasi hizo kwenye vyombo vya habari jana likiwamo gazeti la Mwananchi kwa kuwataka wenye sifa wajitokeze kuomba.

Dar es Salaam. Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetangaza ajira mpya 28 lengo likiwa ni kuifufua kampuni hiyo.

ATCL imetangaza nafasi hizo kwenye vyombo vya habari jana likiwamo gazeti la Mwananchi kwa kuwataka wenye sifa wajitokeze kuomba.

Nafasi hizo zilizotangazwa na ATCL  ni marubani wanne, wahandisi sita na wahudumu 18. 

Mei 12 mwaka huu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye mkutano wa tatu wa Bunge la Bajeti, alisema Serikali imekusudia kuagiza ndege mbili ili kuhakikisha ATCL inainuka katika huduma za usafiri wa anga.

Mbarawa alisema: “ATCL ina wafanyakazi 200, tutaajiri upya wafanyakazi na watakaokuwapo ni wale watakaoendana na idadi ya ndege, hatutaki kuwa na wafanyakazi wanaopiga maneno, lengo letu ni kuifufua ATCL.”