ATE yaanza mchakato wa mwajiri bora

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk Aggrey Mlimuka.

Muktasari:

Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kimefungua pazia la kinyang'anyiro cha kusaka  mwajiri bora wa mwaka, ambaye atatunukiwa tuzo Desemba mwaka huu.

Dar es Salaam. Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kimefungua pazia la kinyang'anyiro cha kusaka  mwajiri bora wa mwaka, ambaye atatunukiwa tuzo Desemba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk Aggrey Mlimuka amesema tuzo hizo za ambazo zimekuwa zikitolewa tangu mwaka 2005 zinalenga kutambua waajiri wenye misingi bora.

Amesema kabla ya kumpata mshindi wa mwaka huu watafanya utafiti kwa kutumia mshauri mwelekezi.