Abiria wa treni kurejeshewa nauli

Muktasari:

Hali hiyo imetokana na hitilafu ya usafiri wa treni juzi usiku.

Dar es Salaam. Zaidi ya abiria 1000 watalipwa nauli zao kama fidia ya kukosa huduma ya treni kutoka stesheni kuelekea Pugu.

Hali hiyo imetokana na hitilafu ya usafiri wa treni juzi usiku.

Shirika la Reli Tanzania (TRL), limesema litawarudishia nauli abiria ambao watahitaji kwa kuwa tayari walishatoa tamko wanaweza kufanya hivyo au kutumia tena tiketi zao kwa siku ya jana.

Ofisa Uhusiano TRL, Midladjy Maez, amesema jumla ya mabehewa 20 ambayo yanatumika na treni hiyo kutoka Stesheni hadi Pugu jana yalikumbwa na adha hiyo licha ya wengi kuamua kutafuta njia mbadala ya kusafiri.