Muktasari:

Tajiri huyo ameelezea imani yake kwa kocha, Antonio Conte akimtaka awasajili Antoine Griezmann na Antonio Rudiger Januari mwakani, huku hali ya baadaye ya mabeki Branislav Ivanovic, Nemanja Matic, Oscar na kiungo Cesc Fabregas ikiwa shakani.

London, England. Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich yuko tayari kuipa klabu hiyo fedha za usajili ili kusuka upya kikosi ambacho msimu huu kinachechemea.

Tajiri huyo ameelezea imani yake kwa kocha, Antonio Conte akimtaka awasajili Antoine Griezmann na Antonio Rudiger Januari mwakani, huku hali ya baadaye ya mabeki Branislav Ivanovic, Nemanja Matic, Oscar na kiungo Cesc Fabregas ikiwa shakani.

Wakati hayo yakiendelea Chelsea, Manchester United ipo tayari kumpa mkataba mpya Juan Mata ili kumbakiza kwenye klabu hiyo ya Old Trafford.  Mata ameanza mazungumzo na kocha wake, Jose Mourinho kuhusu mkataba mpya