Adaiwa kumweka rehani mwenzake Pakistani

Sheria imechukua mkondo wake

Muktasari:

Mwinyi anayedaiwa kumweka rehani Akida Juma, alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana na kusomewa shtaka moja la kusafirisha binadamu.

Dar es Salaam. Mkazi wa Dar es Salaam, Juma Mwinyi anayedaiwa kumweka rehani mwenzake nchini Pakistan, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mwinyi anayedaiwa kumweka rehani Akida Juma, alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana na kusomewa shtaka moja la kusafirisha binadamu.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 17, itakapotajwa tena.