Adaiwa kuua mke kwa wivu wa mapenzi

Muktasari:

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Francis Massawe amesema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi na chanzo chake kinadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Babati/Dodoma. Mwalimu wa Shule ya Msingi Dabil, Tarafa ya Bashnet wilayani Babati, Mkoa wa Manyara, Domitila Gabriel (25) amefariki dunia kwa kukatwa na panga na mumewe baada ya kukutwa akizungumza faragha na mwalimu mwenzake.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Francis Massawe amesema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi na chanzo chake kinadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Massawe siku ya tukio hilo, mwanaume huyo alimkuta mke wake akizungumza na mwalimu mwenzake wa kiume wakiwa peke yao wawili majira ya saa nne usiku, ndipo alipochukua uamuzi wa kumkata panga huku mwalimu mwenzake akikimbia kuepuka kuuawa.