Ahadi ya Magufuli kwa Bakhresa yatimia

Dar es Salaam.  Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limetekeleza agizo la Rais John Magufuli la kupeleka umeme katika katika kiwanda cha Bakhresa wilayani Mkuranga.

Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba amesema kuwa agizo hilo limekamilika Novemba 30, 2016 ndani ya muda aliotoa Rais Magufuli.

Amesema umeme tayari umefika lakini Bakhresa alikuwa hajaweka miundombinu ya kuunganisha na ameagiza vifaa vinavyotakiwa ili kupata umeme huo.

Rais Magufuli alipotembelea kiwanda hicho cha juisi alitoa miezi miwili kwa Tanesco kufikisha umeme katika eneo hilo.