Ahukumiwa miaka 20 jela kwa meno ya tembo

Muktasari:

  • Mshtakiwa huyo anadaiwa kukutwa na  vipande hivyo vyenye uzito wa kilo 24 vyenye thamani ya Sh21 milioni  mali ya Serikali.
  • Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan alisema ametoa hukumu  hiyo baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi saba.

 

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala mkoani hapa,  imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh211 milioni  Said Zomola (30) baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande 14 vya meno ya tembo.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kukutwa na  vipande hivyo vyenye uzito wa kilo 24 vyenye thamani ya Sh21 milioni  mali ya Serikali.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan alisema ametoa hukumu  hiyo baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi saba.

Hata hivyo, wakati hukumu hiyo ikitolewa, mshtakiwa huyo hakuwapo mahakamani baada ya kuruka dhamana.

“Baada ya kuwasikiliza mashahidi hao wote mshtakiwa alitakiwa afike mahakamani kwa ajili ya kutoa utetezi wake, lakini ameshindwa  kwa kuruka dhamana na hivyo mahakama inamtia hatiani kama alivyoshtakiwa pasipo kuwapo,’’ alisema.