Airte Money yatangaza gawio la Sh1.4 bilio kwa wateja, mawakala

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akizungumza na  waandishi wa habri, Dar es Salaam kuhusu gawio la Shilingi 1.4bilioni litakalo gawiwa  wateja wa kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Airtel Tanzania, Isack Nchunda.

Muktasari:

Kampuni ya Airtel Tanzania imetangaza kutoa gawio la Sh1.4 bilioni kwa wateja wake wa huduma ya Airtel Money.


Dar es Salaam. Kampuni ya Airtel Tanzania imetangaza kutoa gawio la Sh1.4 bilioni kwa wateja wake wa huduma ya Airtel Money.

Mkurugenzi wa masoko na Airtel Money, Isack Nchunda amesema gawio hilo litatolewa kwa wateja wote pamoja na mawakala wa Airtel Money waliotumia huduma hiyo kwa miezi mitatu ya kwanza mwaka huu; Junuari mpaka Machi.

“Huwa tunatoa gawio katika kila robo ya mwaka tangu mwaka 2015. Kwa robo ya kwanza mwaka huu tumetenga Sh1.4 bilioni. Wateja wa Airtel Money pamoja na mawakala watakuwa na uhuru wa kuchangua jinsi ya kutumia fedha zao,” amesema Nchunda.

Mpaka Machi, takwimu za Mamlaka ya MAwasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha Airtel Money ilikuwa na wateja milioni 3,923 ambao waliongezeka mpaka milioni 4.07 Juni na kuiweka nafasi ya tatu ikitanguliwa na M-Pesa ilikuwa nao milioni 8.642 na Tigo Pesa milioni 6.979.

Nchunda amesema hayo leo, Oktoba 11 na kubainisha kuwa kila mteja atapokea gawio hilo kulingana na salio analokuwanalo kila siku katika akaunti yake ya Airtel Money.

Tangu Airtel ilipoanza kutoa gawio mpaka sasa, amesema kiasi cha  Sh17 bilioni kimelipwa. Kadri siku zinavyozidi kwenda, huduma za kampuni zinaendelea kuboreshwa na hizi sasa inawaruhusu wateja waliokosea kutuma fedha kusitisha muamala.

Kusitisha muamala uliotumwa kwa makosa, amesema mteja anapiga *150*60# kisha anachagua akaunti yangu na kuchagua rudisha muamala. 

Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Malando amesema kuanzia sasa kila mteja au mawakala wa Airtel Money atapokea gawio kupitia akaunti yake ya Airtel Money.

“Kupitia Airtel Money pekee mteja anaweza kutuma, kupokea na kutoa fedha bure na kufaidi  mikopo ya papo kwa hapo ya Airtel Money Timiza,” amesema Malando.