Airtel yamwaga Sh 3.1 bilioni kwa watumiaji wa Airtel Money

Muktasari:

Pesa hizo wataweza kuzitumia wapendavyo katika mahitaji mbalimbali ikiwemo kununua data na pamoja na kulipia huduma mbali mbali kwa kupitia akaunti zao za Airtel Money.

Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeanza kutoa gawio kwa wateja wake wa Airtel Money katika robo ya kwanza ya mwaka huu kutokana na faida inayotokana kwa kutumia huduma hio.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Uhusano wa Airtel, Jackson Mmbando amesema kampuni yake imetenga gawio la takribani Sh 3.1 bilioni ambazo zinarudishwa kwa wateja na mawakala wa Airtel Money kulingana na matumizi yao ya huduma ya Airtel Money kwenye kutuma na kupokea pesa.

Amesema Airtel imekuwa ikitoa gawio kama hilo kila baada ya miezi mitatu. "Wateja wetu pamoja na mawakala watapata gawio lao kulingana na vile walivyotumia huduma yetu ya Airtel Money kwa hiyo viwango vya gawio watakavyopata kila mteja vitakuwa vinatofautiana kulingana na jinsi mteja alivyotumia kwa wingi."

Mmbando aliongeza kusema kuwa kila mteja atatumiwa gawio lake kupitia akaunti yake ya Airtel Money na anaweza kutumia fedha hizo kwa matumizi mbali mbali kama  vile kulipia huduma ya maji, kulipia Tanesco, kuwatumia ndugu na jamaa au kuzitoa pia kwa matumizi