Airtel yazindua vocha ya Sh200

Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga

Muktasari:

  • Vocha hiyo mpya iliyopewa jina la Tabasamu, inatajwa kuwa itawaongezea wateja wake Tabasamu pale wanapopiga simu au kujiunga na vifurushi vya gharama nafuu.
  • Akiongea wakati wa uzinduzi wa vocha hiyo, Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga amesema:

Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo (Jumanne) imezindua vocha mpya ya muda wa maongezi ya Sh 200 kwa wateja wake wa malipo ya awali.

Vocha hiyo mpya iliyopewa jina la Tabasamu, inatajwa kuwa itawaongezea wateja wake Tabasamu pale wanapopiga simu au kujiunga na vifurushi vya gharama nafuu.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa vocha hiyo, Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga amesema:

“Leo tunajisikia fahari kuzindua na kuitambulisha sokoni vocha ya muda wa maongezi ya shilingi 200 itakayowapatia wateja Tabasamu na uhuru wa kuwasiliana na ndugu jamaa marafiki au wale wajasiriamali kuweza kuitumia kupanga mipango yao wakati wowote mahali popote kwa gharama nafuu.”

Vocha  hiyo mpya itapatikana kwa wachuuzi wote wa vocha za Airtel na kuwawezesha wateja wa mtandao huo na Watanzania wote watakaojiunga na Airtel kumudu gharama za mawasiliano wakati wowote kwa gharama nafuu zaidi.

“Tunatambua mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuendesha shughuli zetu za kila siku na hivyo kuboreshwa kwa viwango vya vocha kutasaidia sana kuchochea upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kwa wote,” amesema.

Amesema kampuni hiyo inataka kuendelea kutoa huduma bora za kibunifu na zenye kukidhi mahitaji ya wateja wake.