Ajali mabasi ya Udart yazua kizaazaa

Mabasi ya mwendokasi yakiwa katika kituo cha Kamu Kimarama Dar es Salaam.Picha na Salim Shao.

Muktasari:

  • Udart imesema mabasi yaliyohusika katika ajali yameshaondolewa, hivyo abiria wataendelea na safari kama kawaida.

Dar es Salaam. Abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka (Udart) wamekwama Kimara kutokana na kukosekana huduma kulikosababishwa na ajali iliyotokea Shekilango, Ubungo.

Vituo vya Udart vilivyoko Mbezi Mwisho hadi Ubungo vimefurika abiria baadhi wakiamua kutafuta usafiri mbadala.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus Bugaywa amesema gari moja liligonga lingine kwa nyuma hivyo kusababisha barabara kutopitika.

Bugaywa amesema baada ya mabasi ya Udart yaliyogongana kuondolewa, hivi sasa wanachofanya ni kuhakikisha abiria wote walio vituoni wanapata usafiri.