Ajali ya Uda, treni yaua na kujeruhi usiku huu Kariakoo

Picha na Mpigapicha wetu.

Muktasari:

  • Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
  • Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.

Dar es Salaam. Ajali imetokea usiku huu kati ya treni na basi la Uda linalofanya safari zake kati ya Kariakoo na Mbagala na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.

Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.

“Ni kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana na hivi ninavyozungumza na wewe naelekea Muhimbili,” amesema Kaimu kamanda huyo.

 

Taarifa zaidi mtaisoma katika Gazeti letu la Mwananchi.