Akana kumpa mwanafunzi ujauzito

Muktasari:

Mkazi wa kijiji cha Goweko amendishwa kizimbani kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa Sekondari.

 


Tabora. Mkazi wa kijiji cha Goweko wilayani Uyui, Ramadhan Batueri leo amepandishwa kizimbani kwa tuhuma ya kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Mwandamizi, Idefonce Mkandala akisaidiana na Wakili James Kiwelu ulidai mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai.

Alidai mshitakiwa ametenda kosa hilo kinyume cha kifungu namba 60A kifungu kidogo cha 3 cha sheria ya elimu sura 353 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 ikisomwa pamoja na sheria namba 4 ya mwaka 2016.

Alidai mtuhumiwa huku akifahamu kufanya hivyo ni kosa alimpa ujauzito mwanafunzi huyo mwenye miaka 17 jina linahifadhiwa.

Mtuhumiwa amekana kosa hilo na shauri hilo limeahirishwa hadi Novemba 6 mwaka huu.