Wednesday, June 13, 2018

VIDEO-Aliyejifungua polisi adai kufuatiliwa

 

By Lilian Lucas,Mwananchi llucas@mwananchi.co.tz

Morogoro. Wakati Spika wa Bunge, Job Ndugai akiagiza ufanyike uchunguzi kuhusu sakata la Amina Mbunda kujifungua katika kituo cha polisi Mang’ula wilayani Kilombero, mwanamke huyo amedai bado anafuatwa na askari waliomkamata.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Morogogo, Mugabo Wekwe alisema hana taarifa hiyo.

Akizungumza na Mwananchi jana, akiwa nyumbani kwake, Amina alisema, majira ya mchana askari alifika nyumbani na kumweleza kwa kuwa siku ya kwanza walifanya upekuzi bila kumsainisha karatasi yoyote, sasa wanamuomba kufanya hivyo.

Mume wa mzazi huyo, Abdallah Mrisho alisema kwamba ameshangazwa na askari huyo kumfuata mkewe na kumtaka kusaini hati hiyo ya upekuzi.

-->