Familia ya Kanye West yapata mtoto wa tatu

Muktasari:

Kim Kardashian ameandika barua fupi ya kutoa taarifa hiyo akisema amekuwa mama kwa mara ya tatu baada ya kujaliwa kupata mtoto mwingine wa kike baada ya North (5) na Saint (3).

Familia ya rapa Kanye West na Kim Kardashian imekaribisha mtoto wa watatu baada ya mwanamke aliyewabebea ujauzito (Surrogate) kujifungua alfajiri ya leo Jumatano mtoto wa kike.

Kim Kardashian ameandika barua fupi ya kutoa taarifa hiyo akisema amekuwa mama kwa mara ya tatu baada ya kujaliwa kupata mtoto mwingine wa kike baada ya North (5) na Saint (3).

Pamoja na kushukuru kujaliwa mtoto amesema kitendo cha kubebewa ujauzito na mwanamke mwingine ni kigumu kwa kuwa alikosa udhibiti wa moja kwa moja wa mtoto wake huyo akiwa tumboni.

“Kuna watu wanadhani kubebewa ujauzito ni jambo rahisi kwa kweli nimepitia wakati mgumu sana kwa kuwa binti yangu alikuwa katika tumbo la mwanamke mwingine,” amesema.

Katika habari nyingine watuamiaji wa mitandao ya kijamii wamelipuka wakisema wanafahamu kuwa aliyebeba ujauzito huo ni mdogo wake Kylie Jenner kwani mwishoni mwa wiki iliyopita alilazwa na kumekuwapo taarifa kuwa amejifungua.

Kwa muda mrefu kuwewapo na tetesi kuwa mwanamke aliyebeba ujauzito wa Kim na Kanye ni mwanafamilia hiyo, Kylie Jenner.

Pamoja na hayo Kim hakuwa mtaja mwanamke aliyewabebea ujauzito na ameeleza kuwa baada ya kujifungua alipewa muda mchache wa kumtazama kisha wakakabidhiwa mtoto wao.